Mkuu wa Wilaya Kibaha Nickson Simon pichani juu alipata maelezo kuhusu nishati safi kutoka kwa Innocent Mayawa wa Kampuni ya Kunismat inayotengeneza kuni mbadala zinazotengenezwa na takataka kavu na mimea.
Na Mwandishi Wetu, Kibaha
Mama lishe na baba Lishe zaidi ya 70 katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani ,
wamepewa mafunzo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kutoka Kampuni ya INTERFINi kwa ushirikiano wa Maestro Afrika na kudhaminiwa na Benki ya CRDB.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon amepongeza Kampuni ya INTERFINi kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika ajenda ya nishati safi ya kupikia
Awali Meneja mradi wa Kampuni ya INTERFINi Pamela Mushi amesema kuwa lengo la Program hiyo ya Mapishi hodari ina lengo la kutunza mazingira na kusisitiza kuwa matumizi ya nishati safi siyo anasa.
Mama lishe Ashura Kituta amesema kuwa wanatarajia mafunzo hayo yatakavyoleta matokeo chanya katika shughuli zao za kila siku na kushukuru kuwa miongoni mwa waliopata mafunzo hayo
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo hawapo pichani.
0 Comments