TARURA WASAINI MIKATABA NA WAKANDARASI PWANI

WAKALA wa Barabara  za Vijijini  na Mjini TARURA wamesaini mkataba wa ujenzi wa barabara  katika viwango tofauti  na  Kampuni  25 za Wakandarasi  Mkoani  Pwani.

Hafla hiyo ya utiaji sani imefanyika  leo Agosti 19 kwa kipindi cha 2024-2025 katika  katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa Pwani.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani Leopold Runji amesema kuwa  fedha hizo zinatoka katika mifuko mbalimbali kama mfuko wa Barabara  ambao utafanya matengenezo ya kawaida  Km.810, matengenezo  sehemu korofi Km338.56  matengenezo  ya vipindi maalumu Km.77.34, ujenzi wa Makaravati  mistari 80, ujenzi wa box  culvert 3.

Mhandisi Runji amesema kuwa  fedha za mfuko wa jimbo watatengeneza  na kufanya ukarabati na ujenzi   wa barabara  mbalimbali  kama ujenzi wa barabara   za kiwango cha lami Km.1.35  barabara kiwango chachangarawe Km.52.15  ujenzi wa makaravati.

"Lengo kuu la TARURA  Mkoa wa Pwani ni kuhakikisha  kuwa  mikataba yote itakayosainiwa na  Wakandarasi wote kwa pamoja  wanakwenda  kuanza utekelezaji wa kazi hizi  haraka iwezekanavyo
kwa kuzingatia  kanuni, sheria  na taratibu zilizowekwa" amesema Mhandisi Runji.

Amesema  kuwa  kwa Mkoa wa  Pwani bajeti ya fedha imeidhinishwa  kutoka katika vyanzo mbalimbali iliwemo mfuko wa barabara  jimbo ,tozo na mfuko wamaendeleo (Development RF) ambapo zote kwa jumla ni 31,475,786,735.93.

Runji amesema kuwa ofisi ya TARURA Mkoa wa Pwani imepokea  maelekezo  kutoka TARURA Makao Makuu kuhusu utekelezaji  wa mpango wa  manunuzi wa kazi za matengenezo  ukarabati na ujenzi wa  barabara  2024-25.

Akizungumza  katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewataka Wakandarasi  hao kutekeleza kazi zao ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi kwa wakati na kwatika kipindi cha 2025 Dkt.Rais Samia Suluhu Hassan  arakapopita asipokee malalamiko  kutoka kwa wananchi  nabadala yake apokee shukrani kwa kuufungua Mkoa wa kumaliza ujenzi wa barabara  zote ambazo bado hazijalamilika.nawasihi mkaufungue Mkoa kabla ya lile jambo letu.

'Ninyi TARURA mnakauli mbou yenu isemayo  Tumeifungua  Mikoa hivyo nendeni mkaotekeleze ipasavyo  kwani huwezi kuwa na maendeleo ya kiuchumi kama  nchi hajafunguka na hii ni  jitihada  ya maendeleo  na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi" amesema RC Kunenge. 

Kunenge amesema kuwa "Nawapongeza kwa kujitokeza  kufanya kazi hivyo fanyeni  kazi kwa mujibu wa mikataba  yenu sababu mmeomba wenyewe  hii kazi"amesema Kunenge. 
Aidha Kunenge  amesema kuwa endapo Wakandarasi  hao watapata changamoto katika utekelezaji  wasisite kutoa taarifa katika ngazi za Wakuu wa Wilaya  na vizuri  na wao wakapata nakala ili waweze kufuatilia  na kuulizia  kwani hii mikataba siyo  siri ndiyo maana inasainiwa  eneo la wazi.

"Katekelezeni miradi na pindi inapotekelezwa wananchi wafahamu ili wapunguze malalamiko" amesema Kunenge. 

Runji , amesema kuwa katika utekelezaji wake mfuko wa barabara (Road Fund) utatoa kiasi cha Sh.bilioni 7.5 na bilioni 14.5 zitatoka katika eneo la tozo ya mafuta na mfuko wa Jimbo utatoa Sh.bilioni 4.5 huku fedha za miradi ya maendeleo ya barabara Mil.milioni 300 na mfuko wa dharula utatoa Bil.1.9.

Meneja TARURA Runji amesema kwa awamu ya kwanza imesainiwa mikataba 25 yenye thamani zaidi ya Bil. 11.6 ikiwa ni sawa na asilimia 37 ya bajeti ya mwaka.2024-2025 huku katika  awamu ya pili itasainiwa mikataba iliyosalia.
Akizungumza  kwa niaba ya Kampuni  Lusaka Qs.Amiri Mussa amesema kuwa watakwenda kuhakikisha wanamaliza kazi za ujeni wa barabara hizo ndani ya muda kama ilivyoelekezwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani 

Kamati  ya Ulinzi na Usalama wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu .
Meneja wa TARURA Wilaya ya Kibaha Samuel Ndovani akifuatilia kwa  makini maelekezo  yaliyokuwa wakitolewa kwenye hafla hiyo.
Kutoka Kushoto ni Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Christopher Myava  na Kamishna Msaidizi  wa Polisi (RPC) Pius Lutumo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza  na Wakandarasi  wa Mkoa wa Pwani hawapo pichani.
Meneja wa Wakala wa Ujenzi wa Barabara Mjini na Vijijini TARURA  Mkoa wa Pwani Leopold Runji akizungumza katika hafla hiyo. 
Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani Leopold Runji akimkabidhi  mkataba wa TARURA  Pwani Mkuu  wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge. 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Pwani. 

Post a Comment

0 Comments