HAKUNA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NGORONGORO


NGORONGORO

TAARIFA KWA UMMA

Ngorongoro, Arusha

Tarehe: 18 Agosti, 2024

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) inapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa shughuli za utalii katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro zinaendelea vizuri pamoja na uwepo wa baadhi ya wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo kuandamana leo tarehe

18.08.2024.

Watalii kutoka ndani na nje ya nchi wameendelea na safari zao za kushuhudia vivutio vya utalii ndani ya Hifadhi na Serikali inaendelea kuwahakikishia usalama wao.

Maandamano yaliyoripotiwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii yanaidhihirishia dunia na jumuiya za kimataifa, vyombo vya habari na asasi za kimataifa kwamba ndani ya Hifadhi hiyo hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu na unyanyasaji wa wananchi.

Mamlaka inawahakikishia watalii wote waliopanga safari za kuja Ngorongoro kuwa Serikali itaendelea kusimamia usalama wao wakati wote watakapokuwa ndani ya hifadhi.

Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano kwa Umma,

Hamis Dambaya

Post a Comment

0 Comments