TAJIRI WA ERNIE ELS DESIGN KUJENGA UWANJA WA GOFU ZANZIBAR

 Mkurugenzi wa Zanzibar Amber Resort, Saleh Mohammed Said akitia saini mkataba wa makubaliano na mcheza Gofu duniani Ernie Els ambae ana kampuni ya Ernie Els Design huko Afrika Kusni leo 
 Mkurugenzi wa Zanzibar Amber Resort, Saleh Mohammed Said akiwa pamoja  na mcheza Gofu maarufu duniani Ernie Els ambae ana kampuni ya Ernie Els Design huko Afrika Kusni leo wakati wa utiaji saini makubaliano ya kujenga kiwanja kikubwa cha Gofu Zanzibar
 Mkurugenzi wa Zanzibar Amber Resort, Saleh Mohammed Said akisalimiana  na mcheza Gofu maarufu duniani Ernie Els ambae ana kampuni ya Ernie Els Design huko Afrika Kusni leo wakati wa utiaji saini makubaliano ya kujenga kiwanja kikubwa cha Gofu Zanzibar

‘Kivutio hicho cha utalii kitakua cha kwanza cha aina yake Afrika ya Mashariki’ 

Zanzibar, Tanzania, Afrika ya Mashariki Januari 13, 2017 

Ernie Els Design inafuraha kutangaza imekamilisha makubaliano na Zanzibar Amber Resort na sasa ipo katika hatua ya kwanza ya ujenzi wa kiwanja hicho chenye hadhi ya kimataifa ambacho ni cha kwanza cha aina yake Afrika ya Mashariki.

 Ujenzi unakusudiwa kuanza mwaka 2017. Kiwanja hiki kitakuwa Kaskazini-Mashariki mwa kisiwa cha Zanzibar. Ernie Els anasema, “Kama mbunifu wa viwanja vya gofu, ninajisikia mwenye bahati kubwa kufanya kazi na Zanzibar Amber Resort. Na kutunukiwa baadhi ya mandhari nzuri za Bahari ya Hindi kwa kweli ni fursa kubwa kwetu. 

Wateja wetu na mimi tuna mtazamo unaofanana na ninao uhakika kuwa kazi yetu hapa itaandaa viwango vipya, ikiacha urithi kwa Zanzibar na wachezaji wa gofu kwa ujumla”.

 Kiwanja hichi kitakua mojawapo ya vivutio vingi vitakavyo jengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 638, na kupakana na kilomita 4 za fukwe ya Bahari ya Hindi. Zanzibar Amber Resort itakua na mahoteli matano za kimataifa na nyumba za aina mbali mbali za kifahari. 

Haki miliki za nyumba zitatolewa kwa kipindi cha miaka tisini na tisa (99), na fursa ya nyongeza ya miaka arobaini na tisa (49) kwa wazawa na wageni. 

Zanzibar Amber Resort iko karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ya Zanzibar ambalo linahudumiwa na mashirika ya ndege za Qatar, Uturuki, Condor, Kenya na Ethiopia.

 Brian Thomson & Saleh Said, Wakurugenzi wa Zanzibar Amber Resort waliongezea, “Tulivyoanza mijadala na Ernie, tulibaini kuwa tuna mtazamo unaofanana, wakujenga kujenga kiwanja cha kimataifa cha kipekee ambayo itachochea zaidi uzoefu wa mchezo huu kwa wachezaji wote.

 Uwepo wa kiwanja cha gofu kilicho tengenezwa na Ernie Els Design na hoteli za kimataifa kama vile Anantara na nyinginezo, itachochea utalii wa kifahari wa kipekee kisiwani hapo.

Post a Comment

0 Comments