Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma leo wamejitokeza katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoani humo Salome Kiwaya.
Marehemu alifariki juzi baada ya ajali ya gari mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda nyumbani kwao Njombe ambako ndiko mazishi yatafanyika.
Mama Kiwaya atakumbukwa kwa mchango wake wa kujitoa kwa hali na mali katika shughuli mbalimbali mkoani Dodoma
Kabla ya kuingia kwenye ulingo wa Siasa alikuwa mmfanya kazi wa Ustawishaji Makao Makuu CDA, pia yeye ndiye alikuwa Mratibu wa kwanza shindano la urembo la Miss Dodoma huku akifanikiwa na kumtoa aliyekuwa Miss Tanzania Emily Adolf 1995.
Mbali na urembo pia alikuwa ni mmiliki wa bendi pekee Mkoani Dodoma iliyofahamika kwa jina la SAKISTARS.
Pichani juu marehemu mama Salome Kiwaya enzi za uhai wake.
Blog hii inaungana na wote katika msiba huu bwana alitoa na bwana ametwaa jina lakelihimidiwe.
MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA DSM AENDELEA KUTOA MSAADA KWA KAYA
ZENYE UHITAJI MAALUMU
-
January 8,2025
Mwenyekiti wa wazazi, Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Khadija Ally Said,
ameendelea kutimiza ahadi yake ya kugawa viti mwendo kwa watu wenye
m...
2 hours ago
0 Comments