Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama (katikati) akikata utepe kufungua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana leo mkoani Simiyu.
Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka (wa pili kutoka kushoto), Waziri Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Titus Kamani na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia).
Baadhi ya Wanachi wakifuatilia ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere wilayani Bariadi mkoani Simiyu leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista
Muhagama akipata maelezo kuhusiana na Elimu ya Mpiga Kura alipotembelea Banda
la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo mkoani Simiyu.
Wananchi wilayani Bariadi mkoani Simiyu wakipata elimu ya Mpiga Kura kwenye banda la Maonesho la NEC leo.
Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiandaa vipeperushi vya Elimu ya Mpiga Kura tayari kuwagawia viongozi na wananchi wanaotembelea Banda la Maonesho la NEC.
Na. Aron Msigwa –NEC , Bariadi –Simiyu.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) imepongezwa kwa kuanzisha programu endelevu za utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura kwa kuwafikia
wananchi moja kwa moja katika maeneo yao kote nchini.
Akitoa pongezi hizo
mara baada ya kutembelea Banda la Maonesho la Elimu ya Mpiga Kura la NEC wakati
wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Bariadi mkoani Simiyu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama amesema kuwa hatua ya NEC
kutoa elimu ya mpiga kura kupitia
maonesho hayo inawasaidia wananchi kujifunza masuala mbalimbali kuhusiana na
chaguzi za Tanzania.
“ Nawapongeza Tume ya
Taifa ya Uchaguzi kwa kuanzisha utaratibu huu wa kushiriki maonesho mbalimbali,
mnafanya kazi nzuri, endeleeni hivyo hivyo kuwaelimisha wananchi” Amesema Mhe.
Jenista.
Ameeleza kuwa ushiriki wa NEC katika maadhimisho
ya Wiki ya Vijana unawapa fursa vijana wengi kupata elimu sahihi kuhusu wajibu
wao na majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kuratibu na kusimamia Uchaguzi
wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Kwa upande wake Afisa
Habari wa Idara ya Elimu ya Mpiga Kura ya NEC Bi. Margareth Chambiri
amwemweleza Waziri huyo kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha program endelevu
za kutoa elimu ya mpiga kura kwa kuhakikisha kuwa wananchi moja kwa moja katika
maeneo mbalimbali nchini.
Amesema NEC inatoa
elimu hiyo kwa wananchi ili kuwawezesha kuwa na uelewa sahihi kuhusu utendaji
wa Tume na masuala mbalimbali yanayohusu upigaji wa kura, sheria, taratibu na
kanuni zinazosimamia uchaguzi, taarifa za wapiga kura na maelekezo ya namna ya
kufanya endapo kadi zao za kupigia kura zimepotea au kuharibika, mwananchi
kuhama eneo moja kwenda jingine kutokana na sababu mbalimbali.
Baadhi ya wananchi
waliolitembelea banda la NEC wameeleza kufurahishwa ufafanuzi na elimu ya Mpiga kura inayoendelea kutolewa
na Maofisa wa Tume hiyo kupitia majibu
ya maswali mbalimbali wanayouliza hususan uboreshaji wa Daftari la kudumu la
wapiga kura kwa mujibu wa Sheria ambao utakaowapa fursa ya kuhuisha taarifa zao
pia kupewa elimu kuhusu uendeshaji wa chaguzi mbalimbali hapa nchini.
Aidha, wameiomba Tume
ya Taifa ya Uchaguzi kuendelea kutoa elimu ya Mpiga kura katika maeneo mengine nchini kwa ili kuwawezesha wananchi wengi
zaidi kupata elimu sahihi kuhusu utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
0 Comments