Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh.Gondwe akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini (hawapo pichani) katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Handeni, pembeni ni Afisa madini mkazi Bw. makiyao akifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa.
Mmoja wa wataalamu wa madini akitoa ufafanuzi kidogo kwa wachimbaji wadogo wa madini wilayani handeni
Baadhi ya wachimbaji madini wadogo waliohudhuria kikao hicho
Na Alda Sadango,Afisa Habari wilaya ya Handeni.
Baadhi ya wachimbaji madini wadogo waliohudhuria kikao hicho
Na Alda Sadango,Afisa Habari wilaya ya Handeni.
Mkuu wa wilaya ya Handeni MH. Gondwe amepiga marufuku matumizi ya baruti kwa wachimbaji wa madini wasiokua na leseni, amesema hayo kwenye kikao cha wachimbaji madini wadogo kilichoandaliwa na afisa madini mkazi Bw. Makyao jana.
Amewaeleza wachimbaji kwamba matumizi ya baruti kinyume na taratibu yanaweza kuleta hatari na madhara kwenye suala zima la usalama.
"Nimewapa mamalaka wachimbaji walio na leseni kwa sababu ni kama kitendea kazi kwao lakini pia wanatumia kwa kufuata sheria taratibu na kanuni, Afisa madini mkazi atasimamia magari yanayochukua baruti, kuhakiki maeneo yanayotunzwa baruti hizo na kuhakiki matumizi sahihi ya baruti hizo kabla ya kwenda kuchukua baruti nyingine",alisema DC Gondwe
Alisema kuwa kumekuwepo na ulipuaji wa baruti uliokithiri kwa wachimbaji wasiokua na leseni, hali ambayo imekuwa ikipekelea matatizo ya hapa na pale katika mfumo mzima wa kiutendaji. Mh.Gondwe amewapa muda hadi kufikia Oktoba 13,2016 wawe wamepata leseni za uchimbaji kihalali na kwamba baada ya hapo itaendeshwa oparesheni ya kuwakamata wasiokua na leseni na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Alisema Sheria ya madini inatambulika na adhabu za makosa hayo ni kulipa kiasi cha Milioni 5, kufungwa jela miaka3 au vyote kwa pamoja.Na yeye kama mwenyekiti wa ulinzi na usalama atahakikisha anasimamia hilo kwa maana inakosesha hata serikali mapato kwa kukwepa kulipa kodi.

Aliongeza kuwa kwa kipindi tangu 2014 hadi sasa serikali imepoteza kiasi cha 5.1 bilioni ambapo ni sawa na 1.7 bilioni kila mwaka,hivyo kuna watu wana leseni halali tangu 2014 lakini wameshindwa kuanza kazi kwa sababu ya watu wasiokua na leseni kuwepo maeneo hayo.
Amewaomba wachimbaji wadogo hao ambao wanafuata sheria taratibu na kanuni kushirikiana na uongozi wa wilaya kuhakikisha kwamba wanadhibiti matumizi yasiyo halali ya baruti na wanaokwepa kulipa kodi.
0 Comments