Damian Soul akiwa na Mkurugenzi wa Save The Children Sharon Kassahu.
"Nimetoa wimbo huu maalum kwa ajili ya kuenzi siku ya mtoto wa Afrika ambayo inaadhimishwa kesho
Soul pia amepata fursa ya kufanya kazi na 'Ubongo Kids' kupitia vikatuni venye sauti na kucheza (Annimation).
Aisha kesho ikiwa ndiyo siku ya Mtoto Duniani atakuwa Uwanja wa Jakaya Kikwete ulipo maeneo ya Kidongo Chekundu, Gerezani ambako atazindua rasmi video hiyo.
"Ujumbe uliopo kwenye wimbo ni kuhusi haki za watoto na kusoma bila kuchapwa viboko" alisema Soul.
Nyimbo hiyo itakuwa ikirushwa kupitia kipindi cha 'Ubongo
Kids' kinachorushwa na kituo cha luninga cha TBC ili wazazi waweze kuona na kuufanyia kazi hasa waalimu , ambao wamekuwa katika smstari wa mbele kuchapa wanafunzi wanapokuwa wakiwafundisha.
"Waalimu wafanyie
kazi kuwa watoto wanapaswa kufundishwa kuandika na kuchora bila
kuchapwa fimbo na kupewa adhabu zinazowaachia maumivu" alisema.
Miwsho anawashukuru Save the Children ambao ndiyo wamemwezesha kufanikisha kurekodi wimbo guo katika Audio na Video ikiwa ni pamoja na kuandika baadhi ya maneno kwenye wimbo huo.
0 Comments