SAUTI ZA BUSARA WAITA WASHIRIKI 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Muda ndio huu wa kuomba ushiriki wa tamasha la Sauti za Busara 2017 April 2016 Busara Promotions inawataka wasanii kutoka Tanzania na bara zima la Afrika wanaotaka kufanya onyesho katika tamasha la Sauti za Busara, Zanzibar kuanzia tarehe 9 – 12 Februari 2017.
Vipaumbele vinatolewa kwa wasanii kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na waandaaji wanafanya kila jitihada kuwashawishi wasanii kutoka ukanda huo kushiriki.
Njia za maombi ni rahisi sana. Kuna fomu ya Kiswahili na kingereza kwenye mtandao na kuwasilishwa kabla ya mwisho wa mwezi wa saba, yakiwa yameambatanishwa na nakala ya hivi karibuni na picha.

Jopo la uteuzi litakutana mwezi wa nane kwa ajili ya kupitia maombi yote na wasanii wote watajulishwa mwezi huohuo kama wamechaguliwa au la.
Sauti za Busara ni tamasha la kimataifa, hivyo wasanii, mameneja, waandaaji wa muziki pamoja na waandishi wa habari kutoka sehemu mbalimbali duniani uhudhuria ili kujionea kinachojiri. Kila mwaka tamasha hupokea maombi zaidi ya 600 lakini kuna nafasi arobaini tu, na katika hizo, vikundi 25 vinachaguliwa kuwakilisha Afrika Mashariki na vingine kutoka nchi za Afrika na kwingineko.

Sauti za Busara huonyesha muziki bora wa Afrika. Na huwaleta wasanii mashuhuri wanaowavutia vijana, tamasha huwaalika wasanaii chipukizi, maarufu kutoka mjini na vijijini lakini kwa wale wanaopiga muziki wa laivu tu (hakuna playback).

Kwa ushiriki kwenye Sauti za Busara, wasanii hupata nafasi ya kujitangaza dunia nzima na kwa mwaka mzima katika vituo vya luninga, radio, majarida, tovuti ya tamasha, blogs na tovuti mbalimbali, na machapisho ya nyumbani na ya nje.

Katika tamasha la Sauti za Busara wasanii hupata nafasi ya kuonekana na waandishi wa habari, waandaaji wa matamasha, mameneja wa muziki ambao huja Zanzibar kila mwaka mwezi februari kwa ajili kuangalia vipaji vya wanamuziki wa Afrika Mashariki.

Wasanii wa ndani huonekana baada ya onyesho la Sauti za Busara na kasha hualikwa kufanya maonyesho katika matamasha mengine ndani ya bara la Afrika, Ulaya na Marekani akiwemo Leo Mkanyia, Msafiri Zawose, Jagwa Music, Jahazi Modern Taarab, Bi Kidude (RIP), Tausi Women's Taarab, Maulidi ya Homu ya Mtendeni, Culture Musical Club, X Plastaz, Ifa Band, Makadem and Sarabi (from Kenya) na wengineo.

Post a Comment

0 Comments