WAMILIKI WA MAJENGO WAHIMIZWA KULIPA KODI

Na Skolastika Tweneshe- Maelezo

Wamiliki wa majengo katika Halmashauri ya Ilala wamehimizwa kulipa kodi ya majengo ili kufanikisha maendeleo ya nchi.

 Hayo yamesemwa leo na Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Ilala Tabu Shaibu alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, amesema kuwa wamiliki wa majengo wanapaswa kulipa kodi ndani ya siku 30 tangu anapokuwa amepewa hati ta madai.

Ameongeza kuwa hati hizi uanza kutolewa Julai ya kila mwaka na mlipa kodi anatakiwa kuwa amelipa ifikapo tarehe 31/10 kila mwaka ambapo baada ya mwaka mmoja mlipa kodi atatikwa kulipa faini ya asilimia 25 kwenye kiasi cha kodi ambacho hakijalipwa.

“Kulipa kodi ni lazima kwa maendeleo ya nchi na kodi hii hutozwa chini ya Sheria ya mamlaka za miji (The Urban Authorities Act) namba 2 ya 1983 na marekebisho yake 2002.”

Alisema Tabu Aidha Tabu Shaibu amesema wapo wafanyabiashara wakubwa ambao bado wanadaiwa kodi ya majengo, miongoni mwao ni Air Tanzania Company Limited Tsh 14,124,081.00, Peacok Hotel Tsh 69,960,458.00,

Mohamed Entreprises Limited Tsh 6,274,233.00, Business Printers tsh 6,561,870.00, lamada Hotel & Apartments limited Tsh 24,483,020.00 na Yusuph Mohamed Manji & Salim J Mussa Tsh 21,020,715.00. Kodi ya majengo ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya mapato katika Halmashauri, hivyo ni wajibu wa kila wanananchi kulipa kodi.

Post a Comment

0 Comments