NGUMI ZA KUFUNGULIA MWAKA KUFANYIKA FREDS CORNER MANZESE JANUARY 2

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Selemani Galile 'Selemani Toll' na Zumba Kukwe wanatarajia kuzidunda mwanzoni mwa mwezi ujao katika mpambano wa kufungulia mwaka 2016 kg 75 mpambano utakaofanyika january 2 katika ukumbi wa frends corner manzese

mpambano uho ni wa kumaliza ubishi baada ya mpambano wao wa kwanza miaka mitatu  nyuma kutoka droo ambapo kila bondia amejigamba kumsambaratisha mwenzie

akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mpambano uho ni maalumu kwa ajili ya kumaliza ubishi wa miaka mitatu ya nyuma mpambono walioutoa droo
hata hivyo siku hiyo kutakuwa na mapambano
 ya nguvu ambayo yatawakutanisha mabondia
 mbalimbali ambapo bondia Shomari Milundi atapambana na Hussein Mbonde uku Shedrack Ignas akikumbana na Abdalla Luwanje wakati Mwinyi Mzengela atakumbana na Mohamedi Kashinde na Ramadhani Maonya atakumbana na Said Faraji wakati Kelvin Majiba atakumbana na Ibrahimu Hamis 
Super D alisema kuwa wameandaa mapambano hayo kwa ajili ya kukuza viwango vya mabondia chipkizi na kuimalisha zaidi wale wenye uwezo kwa ajili ya kuwapatia mipambano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi
Super D aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na burudani za nguvu pamoja na ulinzi wa kutosha na ngumi zitaanza mapema ili wapenzi wa mchezo wa masumbwi warudi majumbani mapema wakiwa na furaha ya mchezo utakaochezwa
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile



Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Post a Comment

0 Comments