Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajab Rutengwe
(kulia) akimkaribisha Balozi wa Afika ya Kusini Nchini, Bw. T.D. Mseleku alipomtembelea Ofsini kwake hivi karibuni.
Na Andrew Chimesela Afisa Habari - Morogoro
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajab Rutengwe amesema Pamoja na kuwa Mkoa wa Morogoro
una maeneo makubwa ya ardhi bado maeneo hayo hayajatumika ipasavyo na
kushiwishi wawekezaji kuja kuwekeza Mkoani humo katika Sekta ya kilimo, Viwanda
na Utalii.
Dkt.
Rutengwe ameyasema hayo hivi karibuni wakati wa mazungumzo baina yake na Balozi wa Afrika
ya Kusini Nchini Tanzania Mhe T. D. Mseleku alipomtembelea Ofsini kwake.
Aidha,
alimueleza Balozi Mseleku kuwa eneo ambalo halijatumika kikamilifu katika Sekta
ya kilimo ni kilimo cha umwagiliaji ambacho kwa Mkoa wa Morogoro kinawezekana
kutokana na Mkoa kuwa na mito mingi inayotitirisha maji kipindi chote cha mwaka.
Dkt. Rutengwe alisema, kwa jumla Mkoa wa Morogoro
una maeneo makubwa, yenye rutuba na yanayofaa kwa kilimo. Hata hivyo
alibainisha kuwa ipo ardhi kubwa inayomilikiwa
na Wananchi ambao baadhi yao wameshindwa kuiendeleza na Serikali iko katika mchakato wa kuyachukua maeneo hayo na kuyatoa kwa
wawekezaji watakayoyaendeleza.
“Morogoro
tuna ardhi kubwa na yenye rutuba lakini haijatumika inavyotakiwa, Serekali ipo
mbioni kubadilisha matumizi ya maeneo hayo ili kuwapa wawekezaji wanaoweza
kuitumia ardhi hiyo kikamilifu kwa faida ya wanaMorogoro na taifa” alisema Dkt.
Rutengwe.
Kuhusu
kushawishi wawekezaji wengi kuwekeza Mkoani Morogoro, alisema Mkoa unaandaa kongamano la Uwekezaji ambalo
linatarajiwa kufanyika hivi karibuni kongamano litakalojumuisha Mikoa ya
Morogoro na Pwani.
Kwa
upande wake Balozi wa Afrika ya Kusini Hon. Mseleku alimshukuru Dkt. Rutengwe
kwa kuonesha ushirikiano na dhamira ya dhati ya kuwakaribisha wawekezaji na
kuomba kuendeleza ushirikiano wa pande hizo mbili uliokwishaanza.A
Katika
hatua nyingine Dkt. Rutengwe mara kadhaa
amekuwa akishawishi watendaji katika Mkoa wa Morogoro kuutangaza Mkoa kupitia
vyombo vya Habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kam Blogs ili kuharakisha maendeleo ya Mkoa na watu wake kiuchumi na
kijamii.
0 Comments