Bi. Sajira Mbaga ambaye ni Afisa kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi, akihojiwa nawaandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya wajumbe wa mafunzo hayo wakila kiapo cha uaminifu katika utekelezaji wa zoezi ambalo liko mbele yao. Kushoto ni Hakimu Mkazi Bi. Agnes Ringo
Na Andrew Chimisela
Afisa Habari
Mkoa
wa Morogoro umeanza maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga
kura kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu.
Maandalizi
hayo yameanza jana kwa semina ya siku mbili inayotolewa kwa waratibu wa uboreshaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura katika ngazi ya Mkoa na Wilaya za Mkoa wa
Morogoro.
Semina
hiyo inalenga kutoa Elimu itakayowawezesha kutekeleza jukumu hilo katika
kufanikisha zoezi hilo muhimu. Mafunzo hayo yatahusisha ujazaji wa fomu
zitakazotumika kwenye zoezi zima la uboreshaji la wapiga kura.
Aidha,
yatatolewa mafunzo kwa vitendo yatakayohusu jinsi ya kutumia kifaa cha kisasa yaani
Biometric
Voters Registration (BVR) kinachochukua alama mbalimbali za mpiga kura kwa
lengo la kuondoa uwezekano wa mtu kujiandikisha zaidi ya mara mbili.
Akifungua
mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Dkt. Rajabu Rutengwe kupitia hotuba iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya
Kilosa Mhe. John Henjewele, aliwataka wanasemina kujifunza kwa bidii na
kuhakikisha wanajua utaratibu unaotakiwa kutumika katika kuboresha daftari hilo
la kudumu la wapiga kura.
Dkt.
Rutengwe alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Morogoro kujiandikisha
katika vituo vyao mara muda utakapowadia wa kufanya hivyo. “Naomba kutoa wito kwa
wananchi walio na sifa ya kuwa wapiga kura Mkoani hapa waweze kujitokeza ili
wajiandikishe”. Alisema.
“Aidha,
napenda kuwahakikishia kwamba Serikali Mkoani hapa imedhamiria kuhakikisha
zoezi hili linafanyika kwa ufanisi mkubwa na kufanikiwa” Dkt. Rutengwe
aliongeza.
Naye
Bi. Sajira Mbaga, Afisa kutoka Tume ya Uchaguzi alisema, zoezi la kujiandikisha
kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa Mkoa wa Morogoro, linatarajiwa kuanza
kufanyika Juni 14 mwaka huu na kuongeza kuwa Tume hiyo inaendelea na jitihada
za kuondoa changamoto zilizojitokeza kwenye zoezi hili katika Mikoa mingine ambapo
zoezi hili limekwisha fanyikaA.
0 Comments