WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Qaswida lililoandaliwa na Ulamaa Promotions
Centre litakalofanyika Mei 24 kwenye
viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Ustadhi
Jumanne Ligopora, katika tamasha hilo, wamejipanga kushirikisha madrasa zaidi
ya 50 za jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa.
Aidha, Ligopora alisema hivi sasa wako kwenye mchakato wa kusambaza mialiko
kwa madrasa za Dar es Salaam na mikoani.
“Tunatarajia maelfu ya Waislamu kumiminika kwa wingi katika viwanja vya
Benjamin Mkapa kwa lengo la kupata ladha mbalimbali za Qaswida,” alisema
Ligopora.
Mwenyekiti huyo alisema wameshafanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya
tamasha hilo ambalo anaamini litawapa burudani wote ambao watamwagika uwanjani
hapo.
Cara Terbaik Untuk Menang Judi Sicbo Online
-
Bergabung dalam permainan judi sicbo online yang dapat dimainkan melalui
smartphone, maka tentu saja para pemain bisa melakukan sejumlah taruhan
dengan nya...
Waziri Ndalichako azindua chuo kipya cha VETA Kagera
-
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua
chuo kipya cha VETA Ndolage kilichopo Kamachumu Wilaya ya Muleba mkoani
Kagera k...
0 Comments