WARSHA nyingine ya uandishi
wa filamu inatarajiwa kufanyika wakati wa tamasha la Majahazi la ZIFF
litakalofanyika Julai mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa kwa
vyombo vya habari iliyosainiwa na Daniel Nyalusi, ilisema warsha hiyo itaendeshwa tena na
Maisha Lab ya Uganda .
Alisema maombi kwa wanaotaka
kushiriki yameanza kupokewa na mwisho ni Juni 13.
Nyalusi alisema warsha za
Maisha Lab, zimekuza vipaji vya waandishi wa filamu na wakurugenzi wa filamu
wengi Afrika Mashariki.
“Wanaotaka kusaidiwa katika
hili wanatakiwa kufika ZIFF, Ngome Kongwe Zanzibar, au kutuma maombi yao ya
kusaidiwa kwa barua pepe workshop@ziff.or.tz,” alisema Nyalusi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
wa Maisha Lab, Fibby Kioria, alisema wanatarajia kutoa ‘scholarship’ 60 kwa
mwaka kwa washiriki kutoka nchi zote za Afrika Mashariki, nia ikiwa ni kuongeza
ujuzi na kupanua wigo wa biashara ya utengenezaji wa filamu.
Alisema katika kila warsha,
‘script’ zitashindanishwa na mshindi atapata dola 5,000 za Marekani ili
kumwezesha kutengeneza filamu fupi katika mwaka unaofuata.
Mwaka jana, Nassir Qassimwa
kutoka Tanzania
ndiye aliyeibuka mshindi.
0 Comments