ZAIDI YA WAANDISHI WA HABARI 3200 WAMEPATA ITHIBATI

 

Zaidi ya waandishi Waandishi  wa Habari 3200 kati ya 3900 walioomba Vitambulisho vya Uandishi wa Habari (Press Card)  wamepata  vitambulisho  hivyo baada ya kuthibishwa na Bodi ya Ithibati ya Waadishi wa habari (JAB
Tarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Ithibati kwa watangazaji na Waandishi wa Habari katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji (ABC)  uliofanyika  Februari 13, 2026 Jijini Dodoma.
Mkutano huo wa siku mbili umefanyika  kati ya tarehe 12   hadi  13 Februari  uliofunguliwa  na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo ni wanachama wa Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN), Jumuiya ya  Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), MOAT, NIBA, Wakongwe RTD, Baraza la Habari Tanzania (MCT), MISA Tanzania na EACO.

Post a Comment

0 Comments