Wanamuziki wa kizazai kipya nao hawakubaki nyuma waliimba kama ishara ya heshima kwa Komba
Rais wa Awamu ya pili , Alli Hassan Mwinyi akitoa heshima ya mwisho.
Rais Jakaya Kikwete akipia kwenye jeneza la mwili wa marehemu Kepteni Komba.
Famila ya marehemu Komba wakiwa wameketi nyuma ya jeneza.
Hapa wakiweka mambo sawa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
Baadhi ya wasanii waBongomovie ambao walijitokeza na kuimba wimbo wa kumuaga Komba.
Mbunge wa Kinondoni Mh. Idd Azzan wakwanza kulia akiwa katika viwanja vya Karimjee.
Wasanii wakongwe wakiongozwa na King Kiki , , Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Luizer Mbutu, Kalala Junior na Jose Mara wakiimba kwa uchungu wimbo ambao uliwaliza wengi waliohudhuria kwenye hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akifuta chozi kutokana na mashairi ya wimbo huo ambao awali uliimbw ana marehemu komba ukiwa kati ya nyimbo zake alizotunga wakati wa msiba wa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere.Familia ya Komba wakilia kwa uchungu leo.
Mbunge wa Viti Maalum CCM ,Matha Mlata wakwanza kushoto akiwa na baadhi ya viongozi .
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwenye jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Kepteni Komba.
Rais wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho katika mwili wa marehemu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Anne Samamba Makinda akitoa heshima za mwisho
Katibu Mkuu wa Chama tawala Chama Cha Mapinduzi ,Abdulrahman Kinana akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemi Komba.
Aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyayi Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Komba.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Yusuph Makamba akipangusa machozi.
Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho
Mama Anna Mkapa naye alikuwepo.
Aunt Caroline Sanga wa kwanza kushoto mwenye nyeusi, Mke wa marehemu mama Salome Komba anayefuata wakiwa katika viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam.
Khadija Kopa wapili kushoto akiwa msibani
Baadhi ya watu wakiwa katika viwanja vya Karimjee ambako walihudhuria hafla hiyo
Mjane wa marehemu akibusu mwili wa mume wake marehemu Kepteni John Komba.Marehemu Komba atazikwa kijijini kwao kesho Lituhi mkoani Ruvuma.
NA KHADIJA
KALILI
“NDUGU Wanzania, leo yametimia yaleyaliyoandikwa na
mwenyeezi Mungu, Kiumbe mwadilifu na kipenzi cha watu, Kepteni Komba leo
ametuacha ooh kepteni Komba ooh kwaheri baba, ooh Kepteni Komba kwaheri baba.”
Hii ni
sehemu ya shairi lililoimbwa jana na wasanii wa muziki wa dansi wakiongozwa na
King Kiki akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape
Nnauye, wakati wa kuaga mwili wa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba
katika Ukumbi wa Kareemjee, jijini Dar es Salaam.
Kapteni
Komba aliyefariki dunia jioni ya Februari 28, mwaka huu, mbali ya kuwa
mwanasiasa, ni ni mwalimu kitaaluma na msanii mahiri mwenye kipaji cha aina yake
katika uimbaji ikiwemo uwezo wa kutunga nyimbo mbalimbali za kisiasa na
kiharakati kwa kipindi cha uhai wake.
Hata kibao
hicho kilichoimbwa jana na mzee King Kiki na wasanii wengine wakati wa kuagwa
kwa mwili wa Komba na kuwaliza wengi akiwemo Rais Jakaya Kikwete, kilitungwa
naye kuomboleza msiba wa Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere aliyefariki
Oktoba 14 , 1999.
Alichofanya
King Kiki na nguli wenzake akiwemo Jose Mara, Luizer Mbutu, Kalala Junior, Abdul Salvador ‘Father
Kidevu,’ Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Matha Mlata na Nape, ni kutumbukiza jina
la marehemu (Komba) badala ya Nyerere.
Kwa mguso wa
kibao hicho ambacho kiliwahi kuwaliza wengi na kutikisa vilivyo wakati wa msiba
wa Baba wa Taifa, aina ya maneno yaliyomo ndani yake na ujumbe ulioendana na
mazingira ya msiba huo, jana vilitosha kuwaliza tena wengi akiwemo Rais Kikwete
kwa kushindwa kuvumilia.
Maneno
yaliyotamkwa na Nape kwa staili ya kughani yasemayo ‘nenda Komba kamsalimie
baba wa Taifa, Simba wa Vita (Rashid Kawawa) waambie wameacha
historia ya kutukuka, waliombee taifa letu kwa kipindi hiki, ni maneno
yaliyoibua hisia na simanzi kali kwa umati uliojitokeza.
Wakati
taratibu za kuaga mwili, baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo wasanii, walielezea
kuguswa na msiba huo kubwa zaidi ni pigo kubwa kwa tasnia ya muziki na sanaa
kwa ujumla kutokana na mchango wa Komba wakati wa uhai wake.
Kwa upande
wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) Godfrey
Mngereza, alisema Komba alikuwa ni sawa na mwalimu wa sanaa na kioo cha
wasanii wengi nchini ikiwemo Chuo Cha
Sanaa Cha Bagamoyo.
“Tanzania
One Theatre (TOT), walikuwa wakija kupiga kambi Bagamoyo, hivyo aliweza
kuchukua wasanii wengi wasomi wa Bagamoyo na kuviendeleza vipaji vyao,” alisema
Mngereza na kuongeza kuwa, ni kifo kilichoacha pengo kubwa kwa taifa.
Naye Matha
Mlata, amesema ni kifo kilichowagusa wengi na kuwasihi wasanii wamuunge mkono
Mkurugezni atakayeteuliwa kukiongoza kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT), kwa kumpatia
ushirikiano katika kuenzi mchango wa marehemu Komba.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA), Tallib Cassim alisema wamepoteza
kiongozi na mhimili wa shirikisho kwa sababu alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa
Shiwata, hivyo anafahamu mchango wake wa ndani na nje ya shirikisho hilo.
Talib
alisema, Komba alikuwa mtetezi wa Shiwata hata alipokuwa Bungeni akielezea
malengo ya uwepo nwa chombo hicho kwa wabunge wengi hadi wakaelewa, hivyo kuwa
mwanzo wa kupata baraka zote.
Amewasihi wasanii
kuungana wakiwa na chombo kimoja kitakachowasemea na kupigania maslahi yao
akisema kwa kukosa umoja thabiti, jana walikosa msemaji rasmi wa wasanii katika
msiba huo.
Naye
Sylvester Mujuni ‘Mpoki’ msanii wa vichekesho naye amemlilia Komba kwa kusema msiba ni jambo lenye simanzi
siku zote, hivyo yeye kama msanii ameumia huku akisema kuna wakati alikwaruzana
na Komba kutokana na jinsi alivyokua akimuigiza katika vichekesho vyao vya
Komedi.
Mpoki
alisema, hata yeye alipokuwa akimuigiza, hakua akifanya kwa nia mbaya ni suala
la sanaa jampo ambalo kuna wakati Komba alikua anakasirika, lakini baadaye
akakubaliana na hali halisi.
“Lakini,
mwisho wa siku Komba alikuwa akinielekeza kuwa nisimuigize nikiwa mchafu si
unajua sisi wasanii wakati mwingine tunaigiza huku tukiwa hatujapiga nguo pasi,
akanitaka niweke ndevu, kitambi na nivae ‘smart’ na mimi nilifanya hivyo,”
alisema Mpoki.
Naye Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alimwagia sifa kemkem Komba kwa kusema , nyimbo
zake zilikuza uzalendo katika nchi hii. “Nyimbo
za Komba zilileta changamoto kubwa kila ziliposikika kifo chake ni pigo kubwa kwa wasanii,”
alisema kwa simanzi kubwa.
Mkurugenzi
wa Msama Promotions, Alex Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki
wa injili kupitia uratibu wa matamasha ya Pasaka na Krismasi, alisema kifo
hicho ni pigo na pengo kubwa kwa taifa ambalo ni gumu kuzibika.
Alisema nje
ya sanaa, Komba ni mtu ambaye hakuwa na uroho wa madaraka kwani pamoja na
kupata umaarufu mapema wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, alisubiri hadi
mwaka 2005 alipogombea Ubunge.
Mbunge wa Kinondoni,
Idd Azzan alisema kifo cha Komba ni pigo kwa tasnia nzima ya muziki wa dansi
akisema anamkumbuka sana kwani wakati anaanzisha bendi yake ya Pamo Sound, ndiye
alikua mshauri wake.
“Kubwa zaidi
ninalomkumbuka Komba ni jinsi alivyouinua muziki wa taarab ambapo kama watu
watakumbuka, ulikuwepo ushindano mkubwa kati ya TOT Taarab na Muungano ambapo
wasanii wa kike Khadija Kopa na Nasma Kidogo (marehemu), walikuwa ni mahasimu wa jukwaani,”
alisema.
0 Comments