|
Bondia
Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba wa
kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa kugombea ubingwa wa U.B.O
Africa mpambano uliofanyika jumamosi ya jana Class alinyakuwa ubingwa
huo kwa kushinda kwa Point na sasa Class anashikilia mikanda miwili ya
ubingwa wa Africa W.P.B.F na U.B.O Africa Picha na SUPER D BOXING NEWS |
|
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' askiwa na mikanda yake ya ubingwa wa Africa wa U.B.O na WPBF |
Bondia Fadhili Majiha kushoto
akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa
mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Majiha alishinda
mpambano huo kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto
akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa
kugombea ubingwa wa U.B.O Africa mpambano uliofanyika jumamosi ya jana
Class alinyakuwa ubingwa huo kwa kushinda kwa Point na sasa Class
anashikilia mikanda miwili ya ubingwa wa Africa W.P.B.F na U.B.O Africa
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Cosmas Cheka akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O AFRICA
|
Bondia Ibrahimu
Class 'King Class Mawe' akishangilia ushindi na mashabiki wake baada ya
mpambano wake na Cosmas Cheka na kufanikiwa kumdunda kwa point
Na Mwandishi Wetu
BONDIA machachali wa ngumi za kulipwa
nchini Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ametwaa ubingwa wa U.B.O Africa
mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kumtwanga bondia Cosmas Cheka wa
Morogoro kwa point mpambano wa raundi kumi lililofanyika katika uwanja
wa ndani wa taifa Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
katika mpambano uho ulioanza kwa
mashambilizi kwa kila bondia kumtupia makonde mwenzie kwa ufundi wa ali
ya juu na ulikuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande baada kila mmoja
kujiandaa kwa mda mrefu ata hivyo class alibuka mbabe baada ya raundi
kumi kwisha
katika mipambano mingine iliyopigwa
siku hiyo bondia Fadhili Majiha alimsambalatisha Fransic Miyeyusho kwa
point mpambano mwingine uliowakutanisha bondia chipkizi Vicent Mbilinyi
aliyepambana na Epson John wa Morogoro mpambano uliomalizika kwa sale
wakati bondia Shedrack Ignas alimpiga
bila ya huruma bondia Husein Mbonde kwa K,O ya raundi ya nne ya mpambano
wao nae Saidi Mundi akimpiga kwa point bondia Ramadhani Shauri
aidha wadau wa mchezo wa ngumi
waliofulika kuona mpambano huo wa kistoria wameomba kuwa mapambano hayo
yanatakiwa kuanza mapema kuondoa hadha ya usumbufu wa usafili wakati wa
kutoka na kwenda majumbani kwao kwani wapenzi wa mchezo wengi wa
masumbwi wanategemea daladala kwa usafiri wa kurudi makwao ambapo
ikifika zaidi ya saa sita daladala zinatoweka barabarani |
0 Comments