JOKATE MWEGELO 'KIDOTI' AWAKUMBUKA WATOTO YATIMA TANDALE

 Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akimpa zawadi ya ndala mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma .
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma .
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma .
 
NA MWANDISHI WETU
MISS Tanzania namba mbili 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za kibongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, jana ilitoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Kulea Yatima cha Extrem kilichopo Tandare kwa Bi Mtumwa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mrembo huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti inayojihusisha na masuala ya urembo, alitoa msaada huo kama zawadi yake ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya kwa watoto hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao kujiona wako sawa na wengineo wanaioshi nawazazi wao.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Jokate alisema kuwa ameguswa na kituo hicho ambacho huwa hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira ya eneo hilo.
“Nimefika hapa kutoa msaada kama sehemu ya kuonyesha ninavyoguswa na jamii ya watoto kama hawa, lakini pia nikiwa na lengo la kuwafariji ili nao kujiona ni sehemu ya jamii ya Watanzania,” alisema.
Kidoti alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wenye uwezo, kampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii kwani nao wana haki ya kuishi na ufurahia maisha kama wengine.
Msaada aliokabidhi kwa ushirikiano na kampuni ya Raibow Shell, ni mchele, unga wa sembe, sabuni, jozi za viatu vyenye nembo za Kidoti.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa watoto hao, Mwamvua Jumanne, alitoa pongezi kwa Kidoti na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo kusaidia makundi maalum.
Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mwamvua alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma elimu ya msingi na sekondari, gharama za matibabu pamoja na kukosa watu wa kuwatembelea ili kuwafariji.
 

Post a Comment

0 Comments