UZINDUZI WA ATM ZA SELCOM ZAFANA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA


Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akiwaelekeza kina mama waliotembelea kutoa pesa wakati wa uzinduzi wa mashine ya ATM ya kampuni hiyo ambazo zinatoa  pesa kwa kutumia mitandao mbalimbali ya simu kama M-pesa,tigo pesa,Airtel Money, walipo tembelea katika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere  kushoto ni Ester Kariwa na Joyce Mtema picha na mpiga picha wetu
Mmoja ya wateja waliotembelea banda la kampuni ya Selcom Wireless, Bi,Juliet Benjamin akichukuwa fedha zake katika ATM mashine mpya za kampuni hiyo wakati wa maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere

Wafanyakazi wa Selcom kampuni ya Wireless, wakiwa katika banda lao wakati wa maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere kutoka kushoto ni Juma Mgori Meneja ukuzaji biashara na masoko,Ofisa Mauzo Ally Mbaga na Meneja miradi wa kampuni hiyo Gallus Runyela.

ATM mpya na za kisasa za selcom zawa kivutio kikubwa kwa kampuni ya selcom ambayo imekuwa ikijihusisha na utoaji wa malipo mbalimbali kama vile ving'amuzi na luku mwaka huu imezindua huduma yake mpya ya ATM ambazo zitakuwa zinatoa pesa kwa kutumia mitandao kama Mpesa,Tigo pesa,Airtel Money, na Easy pesa ATM hizo zimevuta hisia nyingi kwa watanzania baada ya kuziona kwa mara ya kwanza katika banda la Selcom na kushudia ATM hizo mpya na za kwanza nchini kutumika kutoa pesa kwa njia ya simu za mkononi

Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akiwaelekeza Goerge Vupembe jinsi ya mashine zinavyofanya kazi.
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu mashine hizo za ATM

Post a Comment

0 Comments