CHARLES SAMA(MCHUMI)
ABDULI M.DOLLAH(DERECTORATE OF BANKING)
IAN BEN MOSHI MTEJA ALIYETEMBELEA BANK KUU
PATRIC A.FATA(PRINCIPLE BANK OFFICER OPERATION DEPARTMENT ZANZIBAR BRANCH)
NEMBO YA BENKIKUU
Na Gloria Matola
Benk kuu ya
Tanzania(BOT) imewataka wananchi
watembelee katika Maonyesho ya Biashara ya 38 (sabasaba) na kutembelea banda
ili kupata uelewa kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Wito huo umetolewa na
mchumi wa Benki hiyo Charles Sama alisema kuwa wananchi wanapaswa kujua
shughuli zinazofanywa na benkikuu kwa kupitia maonyesho hayo ili kufuta dhana
ya upotoshaji uliopo mitaani kuhusiana na noti ya Sh 500 uzi wake una kilevi na
inatumiwa na mateja(wavuta unga) ili kupata stimu.
Alisema kauli hiyo si kweli kwakuwa noti hiyo inachakaa
kutokana na kuwa na mzunguko mkubwa kwa watu wenye kipato cha chini na
kusababisha kuchaka upesi,
Alifafanua kuwa pamoja na kuwa na mzunguko mkubwa na
kusababisha kuchelewa kurudi kwa wakati benki
utunzaji mbaya wa noti hiyo nao unachangia kusababisha kuwa kuharibika.
“Tumegundua utunzaji mbovu wa noti ya Sh 500 hivyo na kuamua
kutengeneza sarafu ambayo itaingia kwenye mzunguko katika mwaka huu wa
fedha,”alisema Sama.
Alifafanua suala la kubadilisha sarafu sio geni kwa Tanzania
kwakuwa awali tulianza na senti na zikabadilishwa hivyo wananchi wasiwe na
mtazamo tofauti kuhusu ubadilishaji huu.
Alisema uvumi wa Tanzania kuthamini sana fedha za kigeni si
wa ukweli kwakuwa dola zinatumika katika maeneo ambayo kuna ushirikiano wa
kimataifa.
“Si kweli kuwa matumizi ya dola ndani ya nchi yanapewa
kipaumbele huo ni mtazamo finyu,sisi hatuwezi kuthamini fedha za watu wa nje na
kuacha za kwetu,”alisema Sama.
Alifafanua matumizi ya fedha za kigeni hutumika katika
hoteli za kitalii na maeneo mengine yanayoingia
watali wa kimataifa.ALisema katika shule za ndani hawawezi kutumia dola watu wote wanatumia pesa ya kitanzania.
Aliongeza suala la fedha za kigeni linaongozwa na sheria ya fedha ya
mwaka 1992 ambayo inatamka bei ya bidhaa na huduma ziwe katia shilingi
ya kitanzania isipokuwa biashara za kigeni na masuala ya kimataifa.
0 Comments