Mwenyekiti
wa Taswa Fc, Majuto Omary, akimtambulisha Rasmi, Bondia Thomas Mashali,
aliyejiunga na timu hiyo siku ya jumamosi katika mazoezi yanayofanyika
kila jumamosi kwenye uwanja wa Chuo cha Ustawi, Kijitonyama jijini Dar
es Salaam.
Katika
kujitambulisha Bondia huyo pia ameweka mikakati ya kuanzisha timu ya
ngumi katika kikosi hicho cha Taswa, ambapo tayari baadhi ya wachezaji
wameonyesha kuvutiwa na mpango huo na kuonyesha nia ya kushiriki
kikamilifu mazoezi hayo ya ngumi yatakayokuwa yakianza mapema siku ya
jumamosi kabla ya kuanza mazoezi ya soka.
Miongoni
mwa wachezaji wa Taswa waliothibitisha kuanza mazoezi ya ngumi na
kushiriki katika baadhi ya mapambano ya ngumi yatakayokuwa yakiandaliwa
na mapromota au Taswa wenyewe, ni pamoja na Hussein, Lukonge, Mkongwe,
Niku, Jimmy, Deusi na Super D
Majuto Omary, akiendelea kumtambulisha Mashali....
0 Comments