Kocha wa wachezaji wa Riadha
waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic
yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw.
Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wanamichezo hao mara baada
ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam jana.
Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa
ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika kuanzia
23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi)
akiwa na baadhi ya wadau wa mchezo wa Riadha waliojitokeza kuwapokea wachezaji
wa mchezo huo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa
ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika kuanzia
23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi)
akiwa na baadhi ya wanamichezo hao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana. Picha na Frank Shija, WHVUM
**********************
Na Frank Shija, WHVUM
Wanamichezo waahidi kuleta medali katika mashindano ya
Olympic yanayotarajia kuanza tarehe 23 Julai jijini Glasgow Scotland.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini jana wakitokea
Ethiopia Kocha wa Timu ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8 Bw. Shaban Hiiti
alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake walioteuliwa katika Timu ya
Taifa kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi waliyoyapata wakiwa nchini
Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa.
Hiiki aliongeza kuwa walipokuwa nchi Ethiopia kwa mazoezi
wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na program za kuwajengea uwezo
wachezaji wake.
“Nimatumaini yangu wachezaji hawa walioteuliwa kujiunga na
wenzao waliokuwa mazoezini katika nchini zingine ambapo wanamichezo wetu
walienda kwa ajili ya mazoezi wataliletea Taifa letu heshima kubwa kwani
wamepikwa wakapikika”. Alisema Kocha huyo.
Aidha kocha huyo amesema kuwa uwepo mazingira mazuri na
vifaa bora vya mazoezi kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua ubora wa wanariadha
hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili nchini Ethiopia.
Kwa upande wake mmoja wa wanariadha ambaye amebahatika
kuitwa kwenye kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo Bw. Alphonce Felix
amesema kuwa anajisikia faraja kuwa miongoni mwa wanamichezo watakao iwakilisha
nchi katika mashindano ya Olympic kupitia mchezo wa riadha.
Alphonce amesema kuwa atatumia ujuzi alioupata nchini
Ethiopia walipokuwa wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini
Ethiopia ikiwa ni jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na kuendeleza
Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo
wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi
katika nchi za Uturuki, China na New Zealand
0 Comments