Mshiriki Kutoka Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha Anneth Paul akipata Huduma ya kutengenezwa Nywele kutoka kwa Mmoja wa Wahudumu wa Saloon Nzuri na Ya kisasa kabisa ya Rino ambapo washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) walipoenda kupendezeshwa kwaajili ya Show ya Mchujo.
Steven
Mapunda mshiriki kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya)
akihudumiwa katika Saloon ya Rino iliyopo Msasani Karibu na Cape Town
Fish Market
Washiriki
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa ndani ya Saloon ya
Kisasa Kabisa ya Rino iliyopo Msasani karibu na Cape Town Fish Market
kwaajili ya kupatiwa huduma zote muhimu za saloon zikiwemo Kutengenezwa
Nywele, Kucha, Uso na Nk kabla ya kwenda kushiriki kwenye Onyesho la
Mchujo ambalo litafanyika jioni ya leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa ambapo leo kuna washiriki wataaga Mashindano hayo.
Saloon
ya Rino iliyopo Msasani karibu na Cape Town Fish Market ndio saloon
pekee ambayo imewapedezesha Washiriki wote 20 wa fainali ya Shindano la
Tanzania Movie Talents (TMT) kabla ya washiriki hao kwenda kushiriki
kwenye Show ya Mchujo ambapo leo washiriki wawili wataaga Mashindano
hayo ambao fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents itafanyika
Mwisho wa Mwezi wa Nane.
Kila
wiki kutakuwa na Show ya mchujo ambapo washiriki wawili watatolewa
katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo fainali yake
itafanyika mwisho wa mwezi wa nane ambapo mshindi mmoja ataondoka na
Kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania na Washindi kumi bora
watafanya filamu ya pamoja na Kunufaika na Filamu hiyo.
Ili
kuweza kuwabakisha washiriki uwapendao unachotakiwa kufanya ni Kuwapigia
kura washiriki kwa Kuandika ujumbe Mfupi wa Maneno kupitia Simu yako
kwa Kuandika neno "TMT" halafu ikifuatiwa kwa namba ya Mshiriki na kutumwa kwenda 15678. MFANO: TMT00 tuma Kwenda 15678
Vilevile
Vipindi vyetu vitaendelea Kurushwa katika Kituo Cha Runinga cha ITV
siku ya Jumamosi saa 4 usiku na Kurudiwa Siku ya Jumapili saa 10 Jioni
na Jumatano saa 5 Usiku.
Ili kuweza Kupata taarifa kuhusiana na Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) nenda kwenye simu yako ya Mkononi andika neno "TMT" halafu tuma kwenda 15678
0 Comments