NA ALLY
KAMWE.
RASMI!
Floyd ‘Money’ Mayweather atapanda tena ulingoni September 13 pale MGM
Grand hotel, Las Vegas kucheza pambano
la marudiano na bondia Marcos Maidana. Kwa sasa ulimwengu wa masumbwi
unaonekana kulihitaji zaidi pambano hili
kuliko pambano la Myweather na Mphilipino Manny Pacquiao.
Hii ni mara
ya pili kwa Mayweather mwenye rekodi ya kushinda mapambano yote 46 aliyocheza
mpaka sasa kukubali kucheza pambano la marudiano! Si kawaida ya Mayweather
kupigana kwa mara ya pili na mpinzani aliyekwishampiga awali, lakini sasa
imekua tofauti na imemlazimu kukubali kutokana na utata uliopo baada ya matokea ya
pambano la awali baina yake na Maidana ambapo Mayweather aliibuka mshindi kwa
tofauti ya pointi.
Pamoja na
matokeo kuonyesha kuwa Mayweather alishinda kwa tofauti ya pointi lakini wadau
wengi wa mchezo huo wanaamini Mayweather alipoteza pambano lile kulingana na
namna Maidana alivyoweza kucheza na kummiliki Mayweather katika raundi zote 12
za pambano lile.
Baada ya
kukubali kucheza pambano hili Floyd
Mayweather anayetafuta rekodi ya dunia
ya kucheza mapambano 50 bila kupoteza alitoa sababu muhimu ambazo kwa kiasi kikubwa
zimemfanya kutofikiria mara mbili katika uamuzi wake wa kucheza tena pambano la
marudiano na Maidana.
NGUMI 221 ALIZOPIGWA NA MAIDANA
ZAMCHANGANYA!
Huenda wengi
wasilijue hili, lakini ndicho alichokisema bondia huyu sugu wa Kimarekani kuwa makonde 221 aliyopigwa na Maidana katika
pambano lao la kwanza ndio yamemfanya
kukubali tena kupanda tena ulingoni na mkali huyo kutoka Argentina.
Mayweather
alisema kuwa idadi hiyo ya ngumi alizopigwa na Maidana ni idadi kubwa zaidi
kupigwa katika historia yake ya masumbwi hali inayomfanya kujiuliza kila mara
ni vipi Maidana alipata nafasi ya kumpiga idadi hiyo kubwa ya makonde.
Takwimu
zimekua zikionyesha kuwa katika jumla ya makonde 858 yaliyotupwa na Maidana
ambayo ni sawa na asilimia 26, makonde 221 yalifika katika mwili wa Mayweather.
Hiki ndicho kinachompa wazimu Floyd Mayweather
“Alishinda
kwa raundi tatu mpaka nne dhidi yangu, haijawahi kuwa hivyo kabla. Ni lazima
nijiulize ni vipi hali hiyo ilijitokeza” Alisema Mayweather
MASHABIKI WANAMPA ‘STRESS’,
Heshima
imeshuka! Ndivyo anavyoamini Mayweather baada ya kuwepo kwa minong’ono mingi ya
watu kudai kuwa alipendelewa katika pambano lake la awali. Wadau wengi wa
mchezo huo wamekuwa wakiamini kuwa Mayweather alibebwa na majaji wakati wa ugawaji pointi katika pambano lao la
awali jambo linaloonekana kumnyima raha bondia huyo.
“ watu
wameshindwa kuulewa mchezo wa ngumi, wametazama kwenye raundi tatu za mwanzo na
kutoka maamuzi yao, hakuna anayejua nini kiliendelea kwenye raundi 9 zilizobaki. Nilishinda, na nitashinda
tena ili kumaliza utata huu” alisema
Mayweather kuonyeshwa kukerwa na maneno ya watu.
“ Sirudi tena ulingoni kwa ajili yake, narudi
kwa ajili ya mashabiki. Mashabiki wameonyesha kuhitaji sana hili pambano hivyo
sinabudi kukubali. Sikubebwa wala sikubahatisha na nitalithibitisha hilo
September 3” aliongezea mwanamasumbwi
huyo anayeongoza kwa kuwa na mkwanja mrefu zaidi duniani kwa sasa kwa upande wa
wanamichezo
NGEBE ZA MAIDANA ZAMKOSESHA USINGIZI
Dogo
anachonga sana! Tangu kumalizika kwa pambano la awali May 3 mwaka huu, bondia
Marcos Maidana amekuwa akijitapa na kutangaza kuwa yeye ndie aliyestahili
kutangazwa mshindi. Kama wengi wanavyoamini ndivyo Maidana anavyoamini kuwa alimpiga Mayweather.
Jambo hili
linaoneka kumkera sana Mayweather kiasi cha kuamini kuwa bila kurudi ulingoni
kuzichapa tena na Maidana huenda akawa ameacha dosari katika rekodi zake za
masumbwi duniani. Ni lazima aje amfunge mdomo Maidana katika hili
“ ametaka
mechi nyingine, nimekubali. Silalamiki tena kuhusu ‘gloves’ zake. Anadai
alishinda pambano la kwanza, hivyo ni bora aje afanye tena na ‘gloves’ zake
zilezile” alisema Mayweather kuonyesha kuchukizwa na tambo za Maidana.
Awali
Mayweather alionekana kulalamika juu ya ‘gloves’ alizokuwa akizitumia Maidana
kuwa zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya kuongeza uzito wa ngumi lakini sasa
mkali huyo amekubali Maidana arudi tena ulingoni na ‘gloves’ zake zilezile
alizotumia awali.
MAYWEATHER BWANA! ETI
ATATUMIA MBINU ZA WAJERUMANI KWENYE ‘WORLD CUP’.
Haishi mikwara huyu! Baada ya kuwaangalia Wajerumani
wakiwaangamiza Waargentina kwenye dimba la Estadio do Maracana pale nchini
Brazil, Floyd Mayweather amesema safari hii atatumia mfumo uleule wa Wajerumani
katika kumchakaza mpinzani wake Maidana anayetokea kwenye taifa la Argentina.
“ kama walivyofanya Wajerumani, ndicho nitakachokifanya kwa
Muargentina mwingine (akimmaanisha Marcos Maidana)” alitamba Mayweather!
Ni Pambano muhimu kwa Mayweather kwa ajili ya kuzima ngebe
za Maidana, ni pambano muhimu kwa Maidana pia kwa ajili ya kuionyesha dunia
kuwa ni kweli alionewa kwenye mpambano wa awali. Dunia ya masubwi inasubiri
kufika September 13 mwaka huu pale Las Vegas.
Nisisahau, hili pia ni pambano muhimu kwa rafiki yangu
Yassin Ustadh kwa ajili ya kuwaonyesha vijana wake kuwa kupigwa ni sehemu ya
changamoto ya mchezo. Lini Maugo amewahi kuzisifia ngumi alizopigwa na Mashali
ama Mashali kuzisifia ngumi alizopokea kwa
Francis Cheka? Ustadh, ngumi 221
alizopigwa Mayweather zimemrudisha ulingoni tena huku akijilaumu na kujishangaa!
Vipi vijana wako, wanasemaga haya?
MATOKEO YA POINTI ZA MAJAJI
ZILIZOZUA UTATA PAMBANO LA AWALI
MAYWEATHER VS
MAIDANA
JAJI NAMBA 1 JAJI NAMBA 2 JAJI NAMBA 3
117-111, 116-112 114-114
kwa hisani ya gazeti la dimba
0 Comments