ACP-David Misime |
Mnamo
tarehe 20/06/2013 majira ya 19.00 hrs maeneo ya Area ‘E’ Manispaa ya
Dodoma Mheshimiwa MOSES S/O MACHALI, miaka 31, Muha, Mbunge wa Kasulu
Mjini kupitia NCCR – Mageuzi wakati anaelekea nyumbani kwake anakoishi
njiani alikutana na vijana wanne (4) walikouwa amesimama katikati ya
barabara akapiga honi lakini hawakupisha. Aliamua kuwauliza “Jamani
mnasimama katikati ya barabara si nitawagonga?”
Nao wakamjibu: “Wewe si unajifanya motto wa Mbunge, tutakupiga sasa”.
Alipojaribu kupita walipiga gari lake. Ilimbidi ashuke ili atazame kama gari hilo limepata uharibifu. Ndipo
vijana hao wakaanza kumshambulia kwa ngumi na mateke huku naye
akijitahidi kujihami, ndipo wakatokea vijana wawili (2) na kumsaidia.
Kijana mmoja kati ya waliokuwa wanamshambulia Mheshimiwa Machali
‘alimng’ata’ mgongoni kijana aliyekuwa anamsaidia Mheshimiwa Mbunge.
Watuhumiwa
baada ya kuona wamezidiwa nguvu walitimua mbio. Mheshimiwa Machali
aligundua kuwa simu yake ya mkononi wameondoka nayo.
Msako mkali ulifanyika na usiku wa manane watuhumiwa wawili (2) walikamatwa ambao ni:-
1. JEREMIA
S/O LAWRENT MKUDE@ JERRY, Miaka 18, Mkaguru, Mkulima, Mkazi wa Chaduru,
Manispaa ya Dodoma. Huyu amekutwa akiwa na jeraha usoni alilopata
wakati anapambana na Mheshimiwa Mbunge na vijana waliokuwa wanamsaidia.
2. CHARLES S/O CHIKUMBILI, Miaka 22, Mkulima, Mkazi wa Swaswa, Manispaa ya Dodoma.
Watuhumiwa walipokamatwa usiku huo wa manane wamekutwa na misokoto miwili (2) ya bhangi.
0 Comments