Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, ikiwemo Jibondo, Chole, Juani, Kanga na Baleni, wamepata huduma za matibabu ya magonjwa mbalimbali kama vile magonjwa ya macho, masikio, uzazi, magonjwa kwa watoto, wazee na magonjwa mengine, bila kulipia gharama yoyote."Hii ni kambi ya tano tangu tuanze mkakati huu wa kusogeza huduma za madaktari bingwa kwa wananchi, na tutaendelea kufikia maeneo mengine yenye uhitaji kama huu," amesema.
Aidha, ametoa wito kwa wadau wengine kuungana nao katika kuendelea kusogeza huduma za afya kwa wananchi, huku akiipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya sekta ya afya.Amesema kuwa anatambua mchango wa wadau hao kufanikisha kambi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mussa Kitungi amesema kuwa Halmashauri ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta za afya, elimu na maendeleo ili kuendelea kuboresha ustawi wa wananchi wa Wilaya hiyo.
Akitambua mchango wa wadau hao kufanikisha kambi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mussa Kitungi amesema kuwa Halmashauri ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta za afya, elimu na maendeleo ili kuendelea kuboresha ustawi wa wananchi wa Wiaya ya Mafia.






0 Comments