Makamu
wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally
Iddy, akipokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za Baraza la
Wawakilishi za mpira wa miguu na pete kutoka kwa Meneja masoko wa
kinywaji cha Grandmalt Fimbo Mohamed Butallah, wakati wa makabidhiano
yaliyofanyika kwenye ukumbi la baraza la wawakilishi Zanzibar, kushoto
kwake ni mwenyekiti wa timu ya Baraza la wawakilishi mheshimiwa Hamza
Hassan Juma. Picha kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited.
**********************************************
WAKATI HUO HUO:- MAANDALIZI YA TAMASHA LA GRAND MALT YASHIKA KASI ZNZ
Na Mwandishi Wetu
HUKU zikiwa
zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania,
maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo litafanyika katika
Viwanja vya Sahara jijini Mwanza, maandalizi yake yamezidi kupamba moto.
Mratibu wa Tamasha
hilo aliye pia Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky, alisema kwa sasa
kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa tamasha hilo Jumatatu
ijayo.
Kissoky alisema,
tamasha hilo ambalo litakuwa la bure kwa watu wote na kushirikisha mastaa wa
filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake kwani vitu vitakavyofanyika vitakuwa
si vya kawaida.
“Kwa sasa
maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, yaani tunaleta kitu tofauti ambacho
watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa na bumbuwazi kuhusu
kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.
Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini
wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua
kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye
uhakika.
“Tumejipanga katika
hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya
jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi . Tunawakaribisha watu wote wenye
mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo
mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.
Naye Meneja Habari
na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi, alisema, kutokana na ubora wa kinywaji cha
Grand Malt hata tamasha hilo litakuwa la aina yake na litakaloiteka mikoa yote
ya Kanda ya Ziwa.
“Tumeona jinsi wananchi wanavyozipenda filamu za
Tanzania, maarufu kama ‘Bongo Movies’ na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona
wasanii wa filamu ana kwa ana, sasa kazi kwao
kuwashuhudia na kuona tamasha bora zaidi,” alisema.
Tamasha la Filamu
la Grand Malt linatarajiwa kuanza Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu
mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu zote hizo ni kutoka
Tanzania.
Wasanii wakali wa
Bongo Muvi wakiwemo Aunty Ezekiel, Vicent Kigosi ‘Ray’, Jacqueline Wolper, Irene
Uwoya, Jacob Steven ‘JB’, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’na Issa Mussa ‘Cloud’ ni baadhi ya wasanii
walioahidi kufanya kweli pia katika tamasha hilo.
Tamasha hilo la
filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho
kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
0 Comments