Na Elizabeth John
MUIGIZAJI wa filamu nchini, Mohamed Nurdin
‘Chekibudi’ amewashukuru wadau na wapenzi wa kazi zake baada ya kumpokea vizuri
na kazi yake inayokwenda kwa jina la ‘Dikteta’, ambayo imeanza kufanya vizuri
sokoni.
Filamu hiyo inayoonesha ukandamizaji wa familia,
imekamilika na kuingizwa sokoni hivi karibuni, ambapo tayari imeanza kufanya
vizuri katika mauzo baadhi ya maeneo ya
jijini Dar es Salaam, ikisambazwa na
kampuni ya steps Entertaiment.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Chekibudi alisema, filamu hiyo
ameiandaa ili kuonesha ukandamizaji uliopo baadhi ya familia katika maisha ya
kila siku, na amefarijika kuona iko katika wakati mzuri sokoni.
Alisema baada ya kuangalia hilo,
aliamua kuweka wazo lake katika filamu ili kuwafikishia ujumbe watu wengi
zaidi na ikawa kama ni moja ya kazi za wasanii
kuelimisha na kufundisha jamii.
“Unajua unapokuwa msanii unatakiwa kuwa mbunifu
katika mambo mengi na ndiyo maana kila kukicha tunaangalia ni jinsi gani
tutawakumbusha wenzetu matatizo ambayo yanaepukika,” alisema Chekibudi.
0 Comments