MSHIRIKI TOKA ARUSHA ATWAA TUZO YA SJMC MISS TOURISM TANZANIA 2012/13, MEDIA AWARD. ATASOMESHWA CHUO KIKUU




Mshindi wa Tuzo ya Media ya Awards kutoka mkoa wa Arusha(katikati) akiwa na wenzake baada ya kutangazwa mrembo wa Vyombo vya Habari vya SJMC Radio, Tv na Magazeti, hafla ambayo imefanyika kwenye ofisi za Chuo Kijitonyama jijini Dar es salaam. Fainali za Miss Utalii zitafanyika tarhe 6/4/2012/13 katika Viwanja vya Makumbusho.

Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin  akikabidhiwa ua na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya chuo cha uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Drk. Herbert Makoye
Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin akivalishwa Skafu maalum ya ushindi na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye

Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin, Akiwa anasogea Mbele Mara Baada ya Kutangazwa kuwa ndiye mshindi wa Tuzo hiyo.



Mshindi wa Tuzo ya Miss Utalii Tanzania 2012/13-Vipaji aliye vaa Skafu ya Tanzania wa Pili kutoka Kushoto Marry Rutta Miss Utalii Tanzania kutoka Mkoa wa Manyara, Akiwa Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin wa tatu kutoka kushoto, pamoja na washiriki wengine.
 Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye akimtangaza Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin.
 Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award nafasi ya pili kutoka Mkoa wa Rukwa Neema Kafanunzi  Akikabidhiwa Zawadi ya Ua na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye
Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award nafasi ya Tatu Baby Juma kutoka mkoa wa Mtwara Akikabidhiwa Zawadi ya Ua na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye
 Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja Mara baada ya kutangazwa kwa Mshindi wa tuzo ya SJMC Media Award
 Rais wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Erasto G. Chipungahelo akitoa neno la Shukurani kwa Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye ofisini kwake 
 Jopo la majaji wakiwa katika Picha ya Pamoja
 Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakitumbuiza Ngoma za asili wakati wa utoaji wa Tuzo hiyo.
 Washindi sita wakiwa katika Picha ya  Pamoja
 Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye (wa pili kulia), akiwa na Washindi wa watatu wa Tuzo ya Media Awards ya chuo hicho, katikati ni mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo kutoka katika Mkoa wa Arusha.
 Meneja vyombo vya habari vya Mlimani-Mama Edda Sanga(kati) Susanne Mbise(kushoto)na Afisa Masoko wa SJMC Sophia Ndibalema(kulia) wakiwa na Mshindi wa Miss Utalii Tanzania-Tuzo ya Media Awards kutoka mkoa wa Arusha, muda Mfupi baada ya kutangazwa katika Hafla iliyofanyika katika Chuo cha SJMC.
Rais wa Miss Utalii Tanzania wa Kwanza kutoka upande wa kushoto Ndugu Erasto G. Chipungahelo Akiwa Na washindi watatu pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye

 **************
Fainali za Utalii Tanzania zimeendelea kushika kasi kwa warembo kushindania Tuzo mbalimbali za Utalii, Utamaduni, Jamii na za Kuichumi. Jana lilifanyika Shindano la kumpata Mshindi wa Tuzo   ya Habari (Media Award) , Shindano ambalo liloifanyika katika Viunga vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam , Shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma (SJMC) ambao ni wadhamini wakuu wa Tuzo hiyo.
Katika Shindano hilo la Miss Utalii Tanzania 2012/13 Media Award zaidi ya Warembo 30 walipanda jukwaani kwa kuelezea mada ya vivutio vya  Mikoa wanayo wakirisha na kisha Majaji wa Shindano hilo kutoka Shule Kuu ya Waandishi wa Habari na mawasiliano ya Umma walitangaza warembo Sita walioingia katika Sita Bora na Baadae waliulizwa Maswali kila mmoja na swali lake na pia swali la pili lilikuwa ni Swali la Jumla ambapo wote waliulizwa.

Washiriki wote walijibu kwa umahiri na baadae wakapatikana washindi watatu ambapo Mshindi wa kwanza alikuwa ni Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin, Mshindi wa Pili alikuwa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Rukwa Neema Kafanunzi na Mshindi wa tatu alikuwa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Mtwara Baby Juma.
Mshindi wa Tuzo hiyo ya Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award   kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin Alipata zawadi  ya Udhamini wa kusomeshwa katika Shule Kuu hiyo ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kutoa Tuzo, Rais wa Miss Utalii Tanzania aliwashukuru wadhamini wakuu wa Tuzo hiyo ya SJMC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Awards, ambao ni Shule  Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma kwa kutoa Heshima kubwa ya Kumsomesha Mshindi wa Tuzo hiyo katika chuo hicho na kuongeza kuwa Elimu ndio Ufunguo wa Maisha na Hilo ni Jambo muhimu katika Taifa letu la Tanzania ambapo  Wasomi zaidi wanahitajika ili Kujenga Taifa na Kukuza Uchumi wa nchi yetu.

Post a Comment

0 Comments