Mtazania Onesmo Ngowi katikati akiwa na baadhi ya maofisa |
LILE Pambano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na watu wengi wa kumpata Mfalme wa
wa bantam wa kimataifa kati ya mabondia Immenuel Naidjala a.k.a Prince kutoka
Namibia na Lesley Sekotswe kutoka Botswana haukuweza kutoa mshondi baada ya
matokeo ya majaji wawili kumpa kila mmoja ushindi wana jaji wa tatu kutoa
draw.
Pambano
hili lilikuwa limeandaliwa na kampuni ya Sunshine Promotions ya bwana Nestor
Tobias na lilikuwa na kila aina ya hamasa baada ya mabondia wote wawili
kuonyesha ufundi wa kurusha makonde.
Rais
wa IBF kutoka Afrika, Ghuba ya Uajemi na mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi
ambaye alikuwa ndiye msimamizi mkuu wa mpambani huu alitangaza kuwa mabondia
wote wawili watakutana tena baada ya kipindi cha mapumziko ya mwezi mmoja ili
kuweza kumpata mshindi wa mkanda huo ambaoni watatu kwa umaarufu katika mukanda
ya ngumi. Mkanda wa kwanza kwa umaarufu ni wa ubingwa wa dunia. Mkanda wa tatu
ni wa ubingwa wa mabara na mkanda wa tatu ni wa ubingwa wa kimataifa ambao ndio
uliokuwa unagombewa na mabanodia hao.
Wakazi
wengi wa jiji la Widhoek na miji mingine ya jirani pamoja nan chi za jirani
walijazana katika hotel ya Widhoek Country Club and Casino kuushughudia
mpambani huo ambao ulikuwa na kila aina ya hamasa.
0 Comments