Wanariadha
kutoka katika mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Dar es salaam na
Arusha wameshathibitisha kushirki katika mbio hizo za kwanza kufanyika
katika historia ya nchi hii tangu uhuru.
Hayo
yamebainishwa na mratibu wa mbio hizo ambaye pia ndiye mwongozaji wa
mbio hizo, Wilhelm Gidabuday akizungumza na LENZI YA MICHEZO kwa njia
ya simu kutoka ARUSHA na kusema kwamba tayari kupitia ofisi za chama cha
Riadha mkoa Arusha (ARAA), wamethibitisha kushiriki mbio hizo.
Gidabuday
alisema kuwa kujitokeza kwa wanariadha hao ni ishara nzuri kwani pamoja
na kwamba ndio mara ya kwanza, kwa muitikio huo, wanatarajia kuwa na
washiriki zaidi ya 500.
“Tumeshapata
maombi kutoka kwa wanariadha kutoka katika mikoa mbalimbali tofauti na
Arusha, kutokana na Taarifa ya ARAA, tayari kuna idadi ya wanariadha mia
tatu, tunatarajia kuwa na wakimbiaji zaidi ya mia tano,” alisema
Gidabuday.
Kuhusu
zoezi la usajili, Gidabuday alisema kuwa zoezi hilo litaanza mapema
baada ya sikuukuu za Pasaka kumalizika na kuongeza kuwa zoezi hilo
litafanyikia katika Ofisi za ARAA, zilizoko katika uwanja wa mpira wa
miguu wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa ada ya sh. 2000 za
Tanzania.
Sokoine
Marathon inatarajia kukukutanisha watu wa kada mbalimbali, wakiwemo
viongozi, wabunge, mawaziri na wananchi kwa ujumla kuadhimisha
kumbukumbu ya kifo cha Hayati Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe
Sokoine yatakayofanyika Aprili 12, wilayani Monduli katika kijiji cha
Enguik Monduli Juu alikozaliwa na kuzikwa.
Mbio
hizo za umbali wa Kilomita 10 na kilomita 2 kutembea na kukimbia
maandalizi yake kwa mujibu wa Waratibu wake mpaka sasa zimeshafikia
hatua nzuri na kwa mujibu wa Waratibu wake, hatua zinazofanyika ni
kufanya mazungumzo na Mgeni Rasmi ambaye kuna uwezekano akawa mmoja wa
viongozi wakuu wa taifa hili.
0 Comments