UTOVU WA NIDHAMU KWA WABUNGE




 Na Bryceson Mathias

Ubabe wa Naibu Spika Job Ndugai hivi karibuni ulibadilika na kusubiri hadi akatoa Kauli na kuwaambia wananchi akisema, “Watanzania jioneeeni utovu wa nidhamu unaofanywa waziwazi”..alisema Ndugai.

Baada ya kusema hayo, Naibu Spika aliposema hivyo alinyamaza akisema waachwe waendelee kupiga kelee hadi wanyamaze ndipo kikao kiendelee, ambapo haikusaidia hadi Mwanasheria wa Serikali Fredrick Werema aliposimama kuokoa Jahazi lakini hakufua Dafu.

Wapenda Haki, Wakristo na wasomaji wa Biblia Takatifu isiyo na uongo kama walivyo baadhi ya wawakilishi wetu walimo bungeni! katika Mithali 14:34 inasema, “  Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wote”.

‘Kila siku inapokuwepo Haki, Taifa huinuliwa, na ndiyo maana katika enzi ya Mwalimu Taifa liliinuliwa kufikia kuitwa Tanzania ni Kisiwa cha Amani. Lakini Haki  inapokosekana, hapo ndipo Dhambi huinuka aibu na utovu ukiasisiwa na wanaoongoza, na kupelekea Utovu wa nidhamu’.

Mstari unaofuata- Mithali 34: 35 ambao hata Ndugai kwa kuwa ni Mkristo amejifunza unasema, “Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.

Ninachotaka niseme bila kumung’unya maneno, kwa Mtazamo wangu! Naona kila kunapotokea Malumbano ya wabunge bungeni, mara nyingi hutokea akiwepo Ndugai kwenye kiti, hii ina maana Upendeleo wake unawaelekea watumwa watendao bila busara!.

Kwa msingi huo inaonesha gadhabu yake saa zote inakuwa juu yao waletao hoka zenye werevu! Na kwa kuwa sasa hakuna mtanzania atakayekula mlenda halafu akadanganywa mlenda huo ni  nyama, hawakai kimya tuu!! Bali wanamuomba Mungu wao ili haki ipatikane na ndipo vurugu hutokea.

Bunge lililopita vurugu na utovu wa nidhamu ulipotokea Ndugai ulikuwa kwenye Kiti, Safari hii tena Utovu wa Nidhamu ambao ulikuwa unaomba watanzania wauone umetokea wewe ukiwa kwenye Kiti, sasa itafika watanzania watajiuliza kwani ukiwepo wewe kwenye kiti kunakuwa na vurugu?

Ni rai yangu kukikumbusha Kiti cha Spika kwamba!! Kwa upendeleo huo mnakotupeleka sasa mkiwa mmekalia Kigoda hicho, ni kwenye kisiwa cha Migogoro, Vurugu na ukosefu wa Nidhamu uliokithiri, nawataka waelewe wao ni vijana wa Juzi, sasa Vijana wa Jana na wa Leo wanajifunza mnachofanya kwa upendeleo; hivyo nao watafanya, muone mkiwa na mikongojo.

Kama Ndugai anataka watanzania waone utovu wa nidhamu unaofanywa na wabunge bungeni, basi watanzania aelewe pia watanzania waona Upendeleo na Ubabe unaofanywa na kiti chake katika kujadili hoja ambazo saa nyingine zingine zinapingwa kwa kulidumaza Taifa badala ya kuliinua.

Ieleweke kwamba, Mtanzania wa leo huwezi ukamuonyesha mtu aliyevaa nguo ya Kaniki, akavaa kofia ya Majani, Klauni ya Lakiri na Mkanda wa Kamba za Mgomba, Viatu vya Magurudumu ya Gari na Fimbo ya Unyasi, ukamwambia huyu ni Askari halafu akakubali! Atakataa.

Ni Busara yangu kumshauri Spika Makinda na Naibu wake, waone umuhimu wa kuwatendea haki kwa sababu hata Baba na Mama wa Familia akianza kuwabagua watoto kwa Jinsia na Uzaliwa wao, kuwa huyu ni mwembamba, Mfupi, Mnene, Mlemavu au Mzima, utakuwa Ubaguzi.

Nzi ni mdudu mchafu, lakini kuna mambo mazuri tunaweza kujifunza kwake. Nzi akitua popote, huanza kuchezesha miguu yake yake kwenda mbele na nyuma, na baadaye ya nyuma, na hatima mbawa za kushoto na kulia!! watalaam wa viumbe wanasema, Nzi huwa anasema, kama unajua ya mbele, yeye anajua ya nyuma, na kama unajua ya nyuma, yeye anajua ya Mbele.

Hitimisho la Ishara na Maelezo yake, wanadai husema kama unajua ya Unaba wa kushoto, yeye anajua ya ubawa wa kulia, na kama unajua ya ubawa wa kushoto, yeye huweza akaruka na kutoa kweye chakula chakula na kukuachia uchafu na hatimae utaugua. Tujifunze na kukubali kushauriwa, badala ya kubisha tuu na kutumia ubabe wa kiti hata kwenye hoja za kweli na msingi kama za akina James Mbatia-NCCR Mageuzi.

Aidha nimepata faraja kwa Kauli ya Ndugai ambayo amesema atamshauri Mkuu wa Kiti Anne Makinda ili aone utaratibu wa kutoa nafasi sawia za kuchangia toka kwa Wabunge wa Chama Tawala na wale wa Upinzani. Ikifanywa hivyo hapo ndipo Haki huinua Taifa.  

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa 

0715-933308

Post a Comment

0 Comments