Vijana waliopewa dhamana ya kupamba eneo la viwanja vya Mnazi Mmoja wakiendelea na kazi hiyo leo, ambapo wanaendelea na ufungaji wa taa ili huduma ya umeme iwepo ya kutosha. |
Vijana waliopewa kazi ya kukata nyasi ndani ya viwanja hivyo wakiendelea na kazi ili kuwe na eneo la kutosha kutoka na wakazi wa jiji la Dar hufurika kwenye viwanja hivyo. |
Maeneo mengine kwenye viwanja hivyo yamewekwa maturubai kwaajili ya kuzuia mvua kama itanyesha |
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania
(Bakwata) limetangaza Maulid ya Mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yatasomwa
usiku wa Januari 24.
Taarifa katika vyombo vya habari
iliyotolewa jana na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Bakwata, Suleiman Lolila,
ilieleza maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika wilayani Mkuranga, Pwani.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa, baada ya
kusomwa kwa Maulid hayo, yatafuatiwa na Baraza la Maulid litakalofanyika
Januari 25, majira ya sasa 9 alasiri.
Taarifa hiyo ilieleza katika maadhimisho
hayo, Waislamu watajifunza mengi juu mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) na
kuyafuata kama ilivyoagizwa katika vitabu vyake vitukufu.
“Bakwata linawataka waumini kuadhimisha
siku hiyo na kupata mawaidha mbalimbali ambayo yatatolewa. Tunawatakia
maandalizi mema ya sikukuu hiyo,” ilieleza taarifa hiyo ya Bakwata.
0 Comments