Boti ya Kikundi cha Mwambao Fishing group iliyopewa jina la” Nani Kama Mama” wakati wa uzinduzi jana ikiondoka katika bandari ya Lindi tayari kwa kazi ya uvuvi (Picha na Freddy Maro)
Mke Wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa msaada vifaa vya kwa
wawakilishi wa kinduchi cha Mwambao Fishing Group katika bandari ya Lindi jana
jioni.
Mke Wa Rais Mama Salma Kikwete na viongozi wengine pamoja na
wawakilishi wa kikundi cha Mwambao Fishing group waki vuta kamba kuzindua rasmi
Boti ya kikundi hicho jana wakati wa sherehe za makabidhiano yaliyofanyika
katika bandari ya Lindi jana jioni
Na Freddy Maro, Lindi
Vijana kikundi cha Mwambao Fishing Group wa
Mji ya Lindi wamemshukuru mke Rais mama Salma Kikwete baada ya
kuwakabidhi Boti ya Uvuvi na vifa vyake katika hafla fupi iliyofanyika
katika bandari ya Lindi jana jioni.
Akisoma risala
kwa niaba ya wanachama wa kikundi hicho, Katibu Msadizi wa kikundi
Bwana Jackson John Mnenje alitoa ahadi ya kutunza boti hiyo na na
kuvitumia kwa malengo waliyojiwekea ikiwamo kununua boti nyingine baada
ya mwaka mmoja kutokana na faida itakayo tokana na biashara za uvuvi.
“Juhudi
alizofanya Mama Salma, zinaonyesha jinsi anavyoguswa na hali ngumu ya
maisha ya Watanzania na dhamira aliyonayo ya kutukwamua kutoka katika
hali hii.Tunamshukuru Mungu kwani leo sisi tumebahatika na kujiunga na
Watanzania wengi wanaofaidika na juhudi zake za kuboresha maisha ya
Watanzania,” wanakikundi hao walisema katika risala hiyo.
Kutokana na
bei kubwa ya vifaa hivyo, vijana hao wamesema kati ka risala yao kuwa,
wasingeweza kamwe kununua vifaa hivyo bila msaada huo uliotolewa na Mama
Salma Kikwete na kwamba utakuwa kichocheo kikubwa cha kukabiliana na
na changamoto za maisha zinazowakabili.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi Msaada huo,mke wa Rais Mama Salma Kikwete alisema
msaada huo ni utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2010 na 2015
inayolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuongeza kuwa ilani hiyo
imetambua kuwa uvuvi ni moja ya sekta za uchumi ambazo hazijapatiwa
msukumo wa kutosha.
“Kuongeza
ufanisi na tija na kubadili maisha ya wavuvi ni moja ya Mapinduzi
yanayolengwa katika ilani ya CCM ya 2010 -2015 na mpango uliopo ni wa
kuimarisha ushirika wa makundi ya ujasiriamali ikiwa ni njia moja kubwa
ya kuwawezesha wananchi wa kawaida kumiliki na kuendesha uchumi,”
alisema Mama Salma.
Mama Salma
amesema kuwa Taasisi anayoingoza ya Wanawake na Maendeleo WAMA
itaendelea kuwasaidi wananchi katika maeneo yao ya kujenga ushirika ulio
imara na unaojitegemea kiuchumi na unaoendeshwa na wao wenyewe katika
misingi wa uwazi na uwajibikaji.
Mama Kikwete
amesema pia kuwa WAMA inalo jukumu la kuhamasisha na kutoa msaada wa
hali na mali kwa wananchi na kuwawezesha kufikia malengo wali yojiwekea
kwa kuwapatia nyenzo na vifaa mbalimbali,lakini wajibu wa kujiendeleza
na kujisimamia unabakia wa watu wenyewe.
Mke wa Rais
amewahimiza wanachama wa Mwambao Fishing group kujenga mshikamano ili
kikundi hicho kipate utulivu utakao wapa fursa ya kupanga mipango ya
kujenga na kuimarisha kikundi na kufanya kazi kwa uwazi,kuaminiana na
kupeana moyo.
0 Comments