Mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mnyika akikabidhi sehemu ya
msaada wa vitu mbalmbali vikiwemo, Shuka, Godoro na Chandarua pamoja na fedha
taslimu kiasi cha sh. laki saba kwa Makamu Mwenyekiti wa timu ya soka ya
Wanawake ya Mburahati Queens, Ridhwan Mkasa kwa ajili ya kuisaidi timu hiyo. Kulia
ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake jimbo la Ubungo (Chadema), Hawa Mwaifunga. (Picha
na Habari Mseto Blog)
Na Elizabeth John
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo,
John Mnyika (Chadema ) amelitaka Shilikisho la saka Tanzania (TFF) kutoa
mchanganuo kwa dola 250 za Marekani zinazotolewa na Shirikisho la soka Duniani
(FIFA) kila mwaka kwa ajili ya kuendeleza soka nchini.
Mnyika aliyasema hayo jijini Dar
es Salaam jana wakati alipokabidhi msaada wa shilingi milion 1.5 pamoja
na godoro moja likijumuishwa kwenye fedha hizo kwa timu ya mpira wa miguu ya
Wanawake ya Mburahati Queens.
“TFF inaulazima wa kutoa
ufafanuzi kuhusu fedha hizo ambazo zinatolewa kwaajili ya kukuza soka la vijana
na wanawake, wanatakiwa kuchanganua kwa kiwango ambacho kulitumika kuanzia Juni
mwaka jana hadi Juni mwaka huu na matumizi yaliyoanza kutumika Julai yanatakiwa
yaelekeze ni kiasi gani kimetengwa kwaajili ya vijana na wanawake,” alisema
Mnyika.
Mburahati Queens ilipewa
msaada huo baada ya timu hiyo kutembelea bungeni mjini Dodoma kwaajili ya kuhamasisha
upatikanaji wa Katiba mpya.
Mnyika alisema shilingi laki
tano zilichangwa na wabunge viti maalumu na kukabidhiwa kwake na Waziri
kivuli wa Habari Utamaduni na Michezo Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ katika
kikao kilichopita.
Pia baada ya kurudi kutoka
bengeni katika kikao kilichopita Mnyika alikusanya michango mingine kwa wadau
wengine na michezo na hadi kufikia kiwango kicho.
Mnyika aliuomba uongozi wa
timu hiyo kuandaa mchezo mwingine wa kuwahamisisha wananchi wa Jimbo la Ubungo kujitokeza
kutoa maoni yao kwa wajumbe wa tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya.
0 Comments