Bendi ya muziki ya dansi ya Sky Light ikitumbuiza katika sherehe za
kutimiza miaka 20 ya Club Bilicanas na miaka 13 ya Clouds FM. (Picha
zote na Habari Mseto Blog)
Sherehe hizo zilipambwa na shamrashamra za aina mbalimabli ikiwemo kukati keki pamoja na kufungua shampeni
Dk. Lilian Mtei akizungumza katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa Clouds FM, Wasiwasi Mwabulambo akizungumza katika hafla hiyo
Tukate keki
Mmoja kati ya wafanyakazi wa kwanza
wakati Bilicanas Club inaanzishwa miaka 20 iliyopita, Monika Victor
akimlisha keki, Dk. Lilian Mtei wakati wa hafla ya kutimiza miaka 20 ya
klabu hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Maandalizi ya keki
Pili Mitemo ambaye
alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye
kwa sasa ni marehemu akipokea keki kutoka kwa Dk. Lilian Mbowe kwa ajili
ya kuwapa wadau waliojitokeza katika hafla hiyo
Mzee Ali Ramadhan Mkude nae akuwa mbali katika mnuso wa Bilicanas Club kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa
DJ Ibrahim Tuwa 'Dj Ibra' akilishwa keki wakati wa hafla hiyo
Dk. Lilian Mtei akimlisha kipande cha keki Meneja Msaidizi wa Vinywaji
wa Club Bilicanas, Amandus Agant wakati wa Birthday ya Bilicanas Club
kutimiza miaka 20.
Monica Victor akigawa keki kwa wadau waliofika katika sherehe hizo.
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akiwa na mmiliki wa blog ya Bongoweekend, Khadija Kalili pamoja na wadau wengine.
Watu wa mataifa mbalimbali wakicheza muziki katika ukumbi wa Bilicanas.
Na Andrew Chale
WADAU mbalimbali wa burudani
usiku wa kuamkia jana walifurahia
kwa pamoja na kula keki ya miaka 20 ya
klabu ya Kimataifa ya Bilicanas na miaka 13, ya Clouds Fm, iliyoambatana na shamrashamra mbalimbali
ndani na nje ya ukumbi huo.
Sherehe hizo ziliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group, Dk. Lilian Mtei ambapo aliwashukuru wadau hao kwa kuwa bega kwa bega na klabu hiyo, tangu 1992. “Tunawashukuru sana kwa kuwa nanyi mara zote inatia faraja kwetu na tutaendelea kutoa huduma bora siku zote|” alisema Mbowe.
Mtei pia aliwashukuru wafanyakazi mbalimbali waliofanikisha
ukumbi huo kufikia hapo na kutoa heshima ya kipekee kwa wafanyakazi waliokuwapo tokea inaanza hadi ilipofikia miaka 20 na
hatimaye kukata keki hiyo.
“Uwepo wa miaka 20, tuna kila sababu ya kuwapongeza
wafanyakazi tuliokuwa nao toka mwanzo
hadi leo, na kwa heshima ya pekee Mama
Victor na Mrs Mitemo ndiyo watakao kata
keki hii” alisema Mtei.
Keki hiyo ilikatwa na wafanyakazi hao Monica
Victor na Pili Mitemo
ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo,
ambaye kwa sasa ni marehemu.
Aidha, kwa upande Clouds FM, iliwakilishwa na Wasiwasi Mwabulambo ambaye alipongeza klabu Bilicanas kwa kuwa mstari wa mbele katika kuinua sanaa nchini hasa kwa kuwasaidia wasaidia wasanii kufikia malengo yao.
Kwa upande wake Ibrahim Tuwa ‘Dj Ibra’ aliyekuwa akisherehesha shughuli hiyo, aliwaomba wadau kuendelea kuwaunga mkono na wataendelea na huduma bora zaidi ha hapo. Dj Ibra alijiunga na Bilicanas tokea 2002,ambapo mpaka sasa ana miaka 10 kwenye klabu hiyo iliyowahi kuwa na madj maarufu waliopita hapo ambao wengi wao wapo kwenye vituo vya televisheni na redio.
0 Comments