TIGO YA KWANZA KUTOA VIFAA VYA NISHATI YA JUA KWA AJILI YA KUCHAJIA SIMU



Ofisa masoko wa kampuni ya Tigo Jacqreliane Nnunduma kushoto  na Meneja Mradi wa Kampuni hiyo Yaya N'dojere pamoja na Ofisa husiano Msaidizi Mariamu Mrangwa wakionesha kifaa cha sora kinavyoweza kufanya kazi ya kuchajishia simu kwa njia ya nishati ya jua


Tigo kuwa ya kwanza kutoa vifaa vya nishati ya jua kwa ajili ya kuchajia simu
Dar es Salaam, Tanzania, 12 Novemba, 2012.  Leo,Tanzania ina idadi kubwa ya watu ambao hawana njia ya moja kwa moja ya kupata umeme, wakati asilimia 50 ya watanzania wanamiliki simu za mkononi. Ili kuchaji simu zao inawalazimu kwenda kwa watu wao wa karibu kama vile ndugu, jamaa, marafiki au wakati mwingine kwenye vibanda na madukani. Kwa vile asilimia kubwa ya watu hawa ni wateja wa Tigo, tumeamua kuyapa maduka yetu  vifaaa vya nishati ya jua vyenye uwezo wa kuchaji simu. Kwa njia hii mteja wa Tigo kamwe hatakuwa na tatizo la simu yake kuishiwa chaji kwa ajili ya kukosa umeme.

Kwa wateja wa Tigo ambao wanaishi mbali na vyanzo vya umeme, huduma hii bunifu inarahisisha na kufanya upatikanaji wa bidhaa za Tigo uwe rahisi, pamoja na kuwapa wateja nishati rafiki na endelevu, kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku . Kwa kupitia vifaa vya nishati ya jua ambavyo vitakuwa vikipatikana katika maduka ya Tigo, Tigo inaendelea kuwajali wateja wake ambao wanaendesha maisha na hata biashara zao katika  maeneo yasiyo na umeme. Wateja watalipia kiasi nafuu cha shilingi 300 kila watakapohitaji kuchaji simu zao.
Kwa wamiliki wa maduka hayo ya Tigo, Tigo inatoa huduma za teknolojia mpya katika soko la Tanzania ili kuwasaidia wajasiriamali kupanua biashara zao na  halikadhalika inaongeza kipato chao.
Wanaohitaji kujisajili kwa ajili ya vifaa wanaweza kutuma barua pepe solar@tigo.co.tz. Kigezo kinachohitajika ni  kutokuwepo kwa umeme kwenye eneo husika au muhusika  awe anauza chaji za simu. Huduma hii itawasaidia wajasiriamali kujipatia chanzo kipya cha mapato kwani kwa wastani wa  malipo ya Tsh. 300  kwa kila huduma anaweza kuingiza  kisasi cha ziada cha Tsh. 90.000 kwa mwezi (kutegemeana na kuchaji simu mara kumi kwa siku) .  
Mradi huu wa bunifu kutoka Tigo umedhamiria kutoa ufumbuzi kwa maeneo yasiyo na umeme Tanzania ili kusaidia ujasiriamali na wakati huohuo kuokoa mazingira kwa kutumia nishati rafiki isiyoathiri mazingira.
Kuhusu Tigo

Tigo ilianza biashara 1994 kama mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania. Sasa inapatikana katika mikoa yote 26 tanzania Bara na Zanzibar. Tigo imejitahidi kuwa na ubunifu katika uendeshwaji wa huduma zake za simu nchini Tanzania kwa kutoa huduma zenye gharama nafuu katika mawasiliano  mpaka katika kutoa huduma za intanet zenye kasi na huduma za fedha kwa njia ya simu kupitia  Tigo Pesa.

Post a Comment

0 Comments