Umwari Neema (22) Mshiriki kutoka Rwanda.
Warembo watakaoziwakilisha Nchi za Rwanda na Kenya katika
mashindano ya Miss East Africa mwaka huu ametangazwa rasmi.
Mrembo atakae iwakilisha Rwanda ni Umwari
Neema (22) ambae ana urefu
wa futi 5.9 ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha Kigali
Institue of Education ( KIE) na pia ni mfanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi
ya Tigo jijini Kigali.
Mrembo atakaeiwakilisha Nchi ya Kenya ni Joan Wambui Ndicho (18) mwenye urefu
wa futi 5.8 na anayetarajia kujiunga na
Chuo kikuu cha Machakos University
College kusomea mambo ya utalii .
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika
tarehe 07 mwezi December mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi,
Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion,
Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa
kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa
njia ya Internet ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na
pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa
Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na
kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam
Imeandikwa na kusainiwa na,
Rena Callist,
EXECUTIVE PRODUCER
EXECUTIVE PRODUCER
MISS EAST AFRICA
BEAUTY PAGEANT
0 Comments