Elie Kamano ‘ General Kamano’ Kulia ambaye ni kutoka nchini Guinea.
Dar es Salaam ,Tanzania
Akizungumza
na waandishi wa habari hawapo pichani ambapo alifichua siri na kusema
kuwa yeye anatoka katika familia ya Machifu nchini humo lakini
amekimbia kuwa Chifu na kukimbilia muziki ambao anasema unampatia
kipato ipasavyo licha ya kwamba alilazimika kufukuzwa nyumbani na
babake mzazi.
"Babangu
hakupenda niwe mwanamuziki ili nije niwe kiongozi kwetu lakini kwa
kuwa kuwa napenda sana muziki nimejikuta nikiziacha mila na kuendelea na
muziki hadi sasa"anasema
Taasisi ya
Kituo cha Utamaduni Cha Ufaransa kesho jioni wameandaa onesho la bure muziki wa
utamaduni wa mwafrika.
Akizungumza
jana katika mkutano na waandishi wa habari Ofisa Habari wa kituo hicho Michael
Shuma aliwataja wasanii watakaonogesha kuwa ni Maryse Ngalula anayetoka Kinshansa Jahuri ya Kidemokrasia ya
Kongo DRC.
Elie Kamano
‘ General Kamano’ anayetoka nchini Guinea anayepiga muziki wake katika miondoko
ya Hip Hop.
Katika
tamasha hilo wasanii hao wawili watatumbuiza mmojammoja na baadaye watatoa
burudani kwa kuimba pamoja.
Wakati
huohuo Koshuma aliongeza kwamba Kituo cha Utamaduni Cha Ufaransa kimekuwa na
utaratibu wa kufanya maonesho la utamaduni.
“Sisi tupo
kwa ajili ya kutangaza Utamaduni wa Mtanzania hivyo nyote mnakaribishwa”.
0 Comments