SAMSUNG YAZINDUA OFA YA MSIMU HUU WA SIKUKUU



 Meneja Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw. Syvester Manyara na Country Trainer wa Samsung Electronics Bw.Joel Laize wakionesha baazi ya simu zilizopo katika Ofa Maalumu ya msimu wa sikukuu ambapo watafanya Droo mbalimbali kwa washindi kujipatia zawadi kem kem kutoka kampuni hiyo 
SAMSUNG YAZINDUA OFA YA MSIMU HUU WA SIKUKUU
“Ni Draw ya zawadi kubwa kwa wateja watakaonunua bidhaa za Samsung”
KAMPUNI ya SAMSUNG Tanzania leo imezindua rasmi ofa maalum ya kipindi hiki cha sikukuu ijulikanayo kama “Samsung Season’s Offer!”. Uzinduzi huu umefanyika katika duka la Samsung lililoko Quality Centre, Dar Es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania Bwana Kishor Kumar alisema, “Ofa hii inalenga kuwazawadia wateja wetu zawadi hizi katika msimu huu wa sikukuu. Ofa hii imeanza rasmi leo Ijumaa tarehe 30 Nov na itaisha Jumamosi tarehe 5 Januari 2013.” Bwana Kishor alielezea zaidi kwamba wateja wote watakaonunua bidhaa za Samsung zilizo katika ofa hii watapata zawadi za papo kwa hapo na pia watapata nafasi ya kujishindia zawadi kubwa katika Draw ya mwisho. Draw ya mwisho itashuhudiwa na wasimamizi kutoka bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha na itafanyika katika duka la Samsung Quality Centre Jumapili tar 06 January mwakani.
Naye meneja usambazaji wa Samsung Mobile Tanzania Bwana Sylvester Manyara alisema kwamba, “Pamoja na bidhaa nyingine za Samsung, bidhaa zilizo katika ofa hii kabambe ni aina ya Galaxy Note 2, Samsung S3, Galaxy Note 10.1, Samsung S Duos, Samsung ACE Duos, Galaxy Pocket na Galaxy Pocket Duos.” Bwana Manyara aliendelea kuelezea kwamba wateja watakaonunua bidhaa za Samsung kipindi hiki watapata kuponi maalum ambazo watajaza na kuzikusanya ili kujaribu bahati yao katika Draw kubwa ya mwisho. Ofa hii inaendeshwa katika maduka ya Dar Es Salaam, na maduka ya Samsung yaliyoko Mbeya, Arusha, Dodoma na Mwanza.
Bwana Kishor Kumar alimaliza kwa kutaja zawadi zitakazotolewa kwamba ni;
1.    Zawadi ya Kwanza; Samsung LED TV ya Inchi 42’.
2.    Zawadi ya Pili; Samsung Galaxy S3 Mobile Phone.
3.    Zawadi ya Tatu; Samsung Galaxy Note 10.1.
4.    Zawadi ya Nne; Samsung Home theatre.
5.    Zawadi ya tano; Samsung Smart Camera.
Pamoja na zawadi hizi, Samsung itatoa zawadi kwa wateja mbalimbali watakaokutwa wakinunua bidhaa za Samsung, miongoni mwa zawadi hizi ni TV tatu za inchi 32 zitakazotolewa moja kila wiki kwa wiki tatu mfululizo kuanzia wiki hii.
Naye bwana Manyara alimaliza kwa kuwashukuru wateja wa Samsung kwa kuchagua bidhaa hizi bora, aliwaomba waendelee kufurahia bidhaa hizi hata baada ya kipindi cha msimu huu wa sikukuu. Aliwakumbusha kwamba miongoni mwa manufaa ya bidhaa za Samsung ni kwamba bidhaa zake ndio tu zina warantii ya miezi 24 yaani miaka miwili. Aliwakumbusha pia kupiga namba ya huduma kwa wateja endapo wakihitaji ufafanuzi kuhusu jambo lolote kuhusu bidhaa za Samsung. Namba ya huduma kwa wateja wa Samsung ni +255 685 88 99 00.
Samsung inaendesha kampeni hii ikiwa ni wiki chache baada ya kufanya maonyesho makubwa ya bidhaa zake jijini Dar Es Salaam yaliyofahamika kama “Samsung Week”. Samsung inafanya pia shughuli nyingi za kujitolea, hususani msaada wa udhamini wa mafunzo kuinua vipaji vya wanariadha katika shule ya Winning Spirit Arusha, msaada kwa shule na matibabu katika kijiji cha Ilmorijo Monduli Arusha na Lyamungu Moshi nk.

Post a Comment

0 Comments