BODI YA UTALII (TTB) YAPEWA CHETI KWA MCHANGO WAKE DHIDI YA MAPAMBANO YA MALARIA KATIKA UZINDUZI WA MPANGO WA KUTOKOMEZA MALARIA UNAOITWA “MALARIA SAFE”






Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuitambua kwa mchango wake katika mapambano dhidi ya Malaria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupambana na ugonjwa huo inayoitwa (Malaria Safe Companys) uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jijini dar es salaam usiku huu ambapo Wizara ya afya inashirikiana na pamoja na taasisi za kimataifa na Makampuni mbalimbali pamoja na Sekta ya michezo, ambapo wadau mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo.Picha na Fullshangweblog.com

Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Hussein Mwinyi akimpongeza Bw. Geofrey Meena baada ya kupokea cheti hicho kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Mzee CHrisant Mzindakaya Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuzalisha nyama ya mkoani Rukwa kwa mchango wake katika kupambana na Malaria nchini.

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wadau makampuni na taasisi mbalimbali wanaopambana na ugonjwa wa malaria nchini mara baada ya uzinduzi huo.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Mzee Salim Mohamed Abeid Bakhressa akitoa ushuhuda kuhusu malaria ilivytokomezwa katika viwanda vyao. 

Mwimbaji nguli wa muziki wa Taarab Khadija Kopa pamoja na kundi lake wakitumbuiza katika hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments