MAHAKAMA
ya Rufani Tanzania, imetengua uamuzi wa Jaji Dk. Fauz Twaib wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, wa kukubali kuufanyia uchunguzi umri wa
msanii Elizabeth Michael 'Lulu'.
Uamuzi
huo wa kuamuru kurudishwa kwa jalada la kesi ya msingi ya mauaji inayomkabili
msanii machachari wa filamu nchini Elizabeth Michael (18), ‘Lulu’, kurudishwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuendelea na mwenendo wa shauri hilo.
Uamuzi
huo ulitolewa leo na jopo la majaji watatu waliokuwa wakisikiliza maombi ya rufani hiyo wakiwa chini ya Mwenyekiti Jaji January Msoffe huku Majaji wengine walioketi kusikiliza maombi
hayo ni Jaji Bernard Luanda na Jaji Edwin Rutakangwa
Naye
Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwasilisha maombi Mahakama ya Rufani akitaka
uamuzi wa Jaji Fauz alioutoa Juni 11, mwaka huu urejewe.
Lulu
anatuhumiwa kwa kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii nyota nchini wa filamu
marehemu msanii Steven Kanumba,aliyefariki
dunia Aprili 7 mwaka huu nyumbani kwake
maeno ya Vatican City , Sinza Jijini Dar es Salaam
Suala
la umri wa Lulu lilizua utata baada ya msanii huyo kusomewa shitaka hilo,
ambapo upande wa Jamhuri ulidai ana umri wa miaka 18, huku mawakili wake
wakidai ana miaka 17.
Mawakili
wanaomtetea Lulu ni Kennedy Fungamtama,
Flugence Massawe na Peter Kibatala, waliomba mahakama ya Kisutu, mbele ya
Hakimu Agustina Mbando, kuufanyia uchunguzi umri wa Lulu na kuomba ashitakiwe
katika Mahakamama ya watoto na kupewa haki haki kama mtoto.
Hakimu
huyo alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kufanya hivyo.
Kutokana
na hilo, mawakili hao waliamua kuwasilisha maombi Mahakama Kuu, ambayo
yalipangwa mbele ya Jaji Twaib Fauz
aliyeamua kwa mamlaka aliyonayo kufanyia uchunguzi umri huo, licha ya maombi
hayo kuwasilishwa yakiwa na kasoro kisheria.
Naibu
Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma, akisoma uamuzi kwa niaba ya jopo
la majaji, alisema uwasilishwaji maombi ulikuwa na kasoro, hata hivyo, liliamua
kulisikiliza kutokana na uzito wa kesi hiyo.
Alisema
Jaji Twaib Fauz alikosea kwa kutumia
vifungu ambavyo havimpi mamlaka ya kuufanyia uchunguzi umri wa Lulu.
"Kama
uamuzi wa Jaji Fauz usingekuwa na dosari, maombi haya yangetupwa lakini
kutokana na kuona dosari hizo ndiyo maana tunaamua kutoa maelekezo kwamba
jalada lirudishwe Kisutu kuendelea na mwenendo wa kesi ya msingi," alisema
Zahra akisoma uamuzi wa jopo hilo.
Majaji
hao walisema Jaji Fauz hakutakiwa kuufanyia uchunguzi umri huo, bali alipaswa
kurejesha jalada Mahakama ya Kisutu na kutoa maelekezo.
Kesi ya msingi ya Lulu inatajwa Mahakama ya Kisutu Oktoba 8 Jumatatu ijayo.
0 Comments