CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pole kwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutokana na vifo vilivyotokea vya watu zaidi 60 baada ya kuzama kwa meli ya Mv Skagit juzi eneo la kisiwa cha Chumbe,Zanzibar.
TASWA inaungana na Watanzania katika kipindi hiki kigumu, huku tukiwaombea waliofariki Mwenyezi Mungu ahifadhi roho zao mahali pema na wale majeruhi awape nguvu wapone haraka waweze kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.
Tunaziomba familia zilizopoteza ndugu zao ziwe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na waamini kwamba huo ni msiba wetu sote na si wao peke yao.
TASWA inaamini wapo wanamichezo waliopoteza maisha kwenye meli hiyo na pia wapo wanamichezo waliopoteza ndugu na jamaa zao, wote tunawapa pole na wawe na moyo wa subira.
(B) MKUTANO MKUU WA MWAKA
Kamati ya Utendaji ya TASWA inatarajia kukutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya chama hicho ikiwemo kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu wa mwaka.
Awali sekretarieti ya TASWA ilipendekeza mkutano huo uwe mwanzoni mwa Agosti, lakini ili kuepuka kuingiliana na mwezi mtukufu wa Ramadhan mkutano huo sasa utafanyika mwishoni mwa Agosti katika tarehe na ukumbi ambao utapangwa na Kamati ya Utendaji.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
20/07/2012
MHANDISI JAMES JUMBE ATIKISA SHINYANGA KWA MOTISHA KUBWA KWA TIMU YA STAND
UNITED!
-
Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe akizungumza
wakati akikabidhi fedha kwa Timu ya Stand United ya Mkoani Shinyanga
#Amwaga V...
2 hours ago
0 Comments