MWANAFUNZI WA AFARIKI KIFO CHA KUTATANISH​A: AOKOTWA MAENEO YA COCO BEACH AKIWA HAJITAMBUI​.

 Mwili wa Marehemu Agnes  ukiwa kanisani tayari kwa heshima ya mwisho katika kanisa la Romani katoliki Mbezi Temboni. Marehemu alizaliwa 29 Julai 1992 na kufa  Julai 16, 2012.
 Mama Mzazi wa Agnes akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa Mwanae.
Hawa ni baadhi ya wanafunzi wenzake aliokuwa akisoma nao katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM na kushoto mwenye shati la mistari ni mwakilishi kutoka wafanyakazi wa IFM.

PICHA HABARI ZIMETUMWA NA HENRY KAPINGA

Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.
Marehemu Agnes B. King'unza alifariki  Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mwili wa Marehemu Agnes King'unza umesafirishwa jana Jioni kwenda Nyumbani kwao Kalenga - Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika leo tarehe 19/07/2012.

Post a Comment

0 Comments