MSAJILI MAHAKAMA KUU APIGA KALENDA KESI YA LULU

Elizabeth Michael 'Lulu'

MSAJILI wa Wilaya wa Mahakama Kuu  Kanda ya Dar es Salaam leo asubuhi Amiri Msumi ameahirisha kesi  inayomkabili msanii wa maigizo nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayetuhumiwa kumuua aliyekuwa msanii nyota wa filamu nchini Steven Charles Kanumba Aprili 7 mwaka huu .

Akiahirisha kesi hiyo jana Msajili huyo  Msumi alisema kutokana na sababu za Jaji anayesikiliza kesi hii katika Mahakama Kuu Jaji Dk. Fauz Twaib kutokuwepo Mahakamani amelazimika kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 20.

"Kwakuwa Jaji Dk. Fauz Twaib ni mwalimu katika chuo cha  Sheria hivyo yuko katika mitihani naahirisha kesi hii hadi tarehe hiyo niliyoitaja ambapo itakuwaja kwa kutajwa".

Post a Comment

0 Comments