HABARI MBALIMBALI KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA TFF LEO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 14, 2012
UHARIBIFU WA VITI UWANJA WA TAIFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo (Machi 14 mwaka huu) limepokea barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo juu uharibifu uliofanyika kutokana na vurugu za washabiki wa Yanga kwenye mechi dhidi ya Azam.
Kwa mujibu wa tathmini ya Serikali, katika vurugu hizo kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jumla ya viti 119 viliharibiwa. Gharama za uharibifu huo ni sh. milioni 5 ambazo Serikali imeagiza zilipwe mara moja.
Kwa vile washabiki wa Yanga ndiyo waliohusika na vurugu na uharibifu huo, gharama hizo zitabebwa na klabu hiyo ili Serikali iweze kufanya ukarabati haraka.
TFF inarudia tena kulaani na kukemea vurugu zinazofanywa na washabiki viwanjani na kusababisha usumbufu, uvunjifu wa amani na uharibifu wa vifaa hasa kutokana na ukweli kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa burudani.
Tunapenda kuwakumbusha washabiki na klabu kuwa vitendo hivyo si vya kistaarabu, hivyo havikubaliki katika mpira wa miguu, na TFF haitasita kuchukua hatua kali kwa wahusika iwapo vitaendelea kutokea viwanjani.
TENGA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI LEO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kesho (Machi 15 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ofisi za TFF.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Post a Comment

0 Comments