NAMIAKA wimbo mpya wa mwamuziki CHE (Che Mundugwao)baada ya kimya cha miaka mitatu mwanamuziki nguli wa muziki wenye vionjo vya asili ya Tanzania na mchanganyiko wa midundo ya muziki wa kisasa (World Music) ametoa wimbo ujaojulikana kwa jina la NAMIAKA ukiwa katika lugha ya Kabila la Wayao ambao ni wenyeji wa Masasi Mtwara ambapo pia kwa asili huyu bwana ndiko anakotokea.
"Nimeamua kuja na mtindo wa Bongo Beat ( Midundo ya Bongo) Jina liloasisiwa bendi ya Super Matimila chini ya marehemu Ramazani Ongala 'Dr Remmy kwenda sambamba na wakati, pia ni katika kuenzi mambo mazuri ya wasanii wakongwe kama Dr. Remmy.Pia nimepata msukumo wa kufanya hivyo kutokana na kuna hawa wadogo zetu wanaopiga muziki katika mtindo wa Bongo Fleva ambayo inapotosha maana asili neno wenye ladha za bongo wakati hakuna sehemu hata moja wenye kuhalalisha usemi huo kitaalamu natukumbuke muziki ni taaluma wenye heshima kubwa duniani.mtu akiibuka na mtindo wa Mduara ,Reggae,Mchiriku,Zouk,Kwaito utasikia wanasema Bongo Fleva hiyo ".Anasema Che
Che na Khadija .
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Samuel Sitta akiwa meza kuu katika hafala inayofanyika mara moja kila mwaka ya Bonanza la Waandishi wa Habari lililofanyika Jumamosi kwenye ufukwe wa Msasani na kuandaliwa na Chama Cha Waandishi wa Habari (TASWA), na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania i( TBL)ambapo waandishi kutoka katika vyombo mbalimbali walijumuika pamoja katika Bonanza hilo.
Akizungumza katika Bonanza hilo Sitta alisema Viongozi walioingia madarakani kwa mgongo wa rushwa , kutumia mitishamba na wenye malengo fulani ndiyo waliyoifikisha michezo ya Tanzania hapa ilipo huku soka likiwa kama kichwa cha mwendawazimu.
Aliongeza kwa kusema kuwa Tanzania imekuwa nyuma katika kila mchezo na hiyo ni kutokana na kuwa na viongozi wasiokuwa na dira.
"Tuko nyuma sana, katika soka hali ni mbaya, riadha kidogo lakini ngumi, kikapu mwaka jana nilikuwa mgeni rasmi pale Uwanja wa Ndani wa Taifa katika fainali hali ikawa mbaya , haiwezekani Watanzania Mil45 tukose watu wenye vipaji" .
"Haiwezekani vinchi vidogo kama Afrika ya Kati Chad waiuke na kuonekana zinatisha kuliko sisi sasa nyie waandishi wa habari wapasheni msiwe watu wa kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa"
Baadhi ya wanahabari wakiserebuka na muziki wa bendi ya FM Academia ambayo ndiyo waliotoa burudani.
Oliver Albert wa Mwananchi Communication na Clezencia Tryphone 'Tasha' wakijiachia katika bonanza hilo.
Kutoka kulia ni Khadija Kalili Tanzania Daima/ Bongoweekend.blogspot.com na Mwanamkasi Jumbe kutoka Kampuni ya Mwananchi Communication.
Wa kwanza kushoto ni Kija Yunus mtangazaji wa Runinga ya EATV pia mwana libeneke katika Afrokija.blogspot.com.
Baadhi ya wanamuziki wa bendi ya FM Academia wakiwa jukwaani huku Cecy Jeremiah wa Redio Uhuru akijaribu kwenda nao sambamba
Ester Mbussi Jamhuri na Happiness Katabazi Tanzania Daima
Khadija&Ester .
Zainab Kihate, Khadija , Somoe na Mdau .
Kutoka kulia ni Khadija, Elizabeth John, Happiness Katabazi, Mwali Ibrahimu (Majira), Nasra Abdallah, Maria Kayala na Asha Bani wote (Tanzania Daima)
Angel Msangi TBC1 na Khadija
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL , Doris Malulu, Tullo Chambo Tanzania Daima na Khadija.
0 Comments