RIP KANAL MUAMMAR GADDAFI


SIRTE, Libya
 ALIYEKUWA kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi (69) ameuuawa katika mapambano makali yaliyokuwa yakifanyika katika ngome ya mwisho ya kiongozi huyo ya jiji la Sirte.
Kiongozi huyo aliyeitawala Libya kwa zaidi ya miaka 42 akiishi katika maisha ya kifahari lakini ameuawa leo mchana  katika makaravati ya mitaro alikokuwa amejificha wakati walipokuwa wakishambuliana vikosi vya NTC .
Gadaffi kiongozi ambaye aliamini wananchi wake kumpenda na hata kuwa tayari kumlinda kwa hatari yoyote ameuawa na vikosi vya raia wanchi yake waliomshambulia katika maficho yake.
Gadafi ameuawa akiwa katika mavazi ya kijeshi, ambako alikuwa katika mapigano na vikosi vyake vilipozidiwa na kuzingirwa Gadaffi alisikika akilia kwa sauti iliyotoka kwenye makaravati akisema 'msiniue', ‘msiniue’. Taarifa zinasema kuwa pamoja na kujitetea kwa kiongozi huyo lakini vikosi vya NTC viliendelea kumshambulia katika maficho hayo na kumsababishia kifo baada ya kupigwa risasi nyingi kichwani na mwilini. kifo cha Muammar Gaddafi kimethibitishwa na Waziri Mkuu wa Serikali ya mpito ya wapiganaji wa NTC, Mahmoud Jibril.
Waziri huyo alisema kuwa Gaddafi kabla ya kuawa alipigwa risasi ya mguu iliyomsababisha kushindwa kuinuka na kubaki chini ambako alishambuliwa mfululizo zilizomjeruhi vibaya mwilini mwake na hatimnaye kuuawa. Inadaiwa kwamba Gadaffi alikamatwa mafichoni kwake baada ya kupewa taarifa mahali ambako alikuwa na hapo ndipo vikosi hivyo vilihamishia mashambulizi yake.
Katika karavati alilokuwa amejificha wananchi wa Libya waliliandika kwa maandishi ya  kiarabu yaliyokuwa  na maneno maarufu ambayo  Gadafi  na alipenda kuyatumia kwa wapinzani wake wa kisiasa kwa kuwaita Panya. Maandishi hayo yalikuwa yakisomeka kuwa 'Hili ni eneo la panya Gaddafi, Mungu Mkubwa'.Wanajeshi wa NTC wamesema kuwa walivamia eneo hilo baada ya kupewa taarifa wakiwa na magari matano yaliyokuwa  yamebeba wanajeshi muda wa asubuhi kwa ajili ya shambuilizi hilo.
Akizungumzia namna walivyomkamata mmoja wa wapiganaji, Mohammed Al Bibi alisema Kanali huyo alipokuwa akipigwa risasi alikuwa akisikika akilalamika 'msiniue, msiniue’ kama mtu aliyekuwa akikusudia kutaka kusalimu amri.Aliongeza kuwa pamoja na kilio hicho lakini vikosi vya NTC viliendelea na mashambulizi katika mguu wake na baadaye mwili mzima. Gaddafi na familia yake wanadaiwa kukimbia katika jiji la Tripoli tangu NATO  na na vikosi hivyo kutangaza kukaribia kuingia katika jiji hilo Agosti mwaka huu.
Kuuawa kwa Gaddafi kumekuja baada ya wanamapinduzi wa NTC kutangaza kulidhibiti jiji la Sirte hapo jana.Gaddafi alikuwa ameripotiwa kutakiwa kushtakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ili afikishwe mahakamani kujibu mashtaka ya jinai. 

Marehemu Kanali Muammar Gaddafi enzi za uhai wake.

Post a Comment

0 Comments