JUMAMOSI iliyopita nilipata fursa ya kuwa kati ya wanahabari wachache waliobahatika kufika mkoani Shinyanga na kuwa sambamba katika shindano la Vodacom Mwanza Cycle Challenge 2011 ambapo wadhamini wenza walikuwa Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Malta Guiness.Pichani ni washindani wakiwa katika shindano ambapo kulia ni Minde kutoka Shinyanga aliyeibuka kuwa mshindi wa 2 akiwa na mmoja wa wakimbiaji kutoka timu ya Arusha jina halikupatikana wakienda sambamba hapa wakitoka Shinyanga kwenda Mwanza.
Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza akimkabidhi zawadi ya sh. mil.1.5 mshindi wa kwanza wa mbio ndefu za baikeli za kilomita 196.Kushoto ni Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Ziwa , Steven Kingu na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Serengeti ambao walikuwa wadhamini wenza Ephraim Mafuru na Meneja wa Kinywaji kisichokuwa na Kilevi ambacho kilidhamini Maurice Njowoka.
Hapa wachezaji wakipanda nguvu kwa kunywa Malta Guiness kabla ya kuanza mbio wakiwa Busanda Shinyanga.
Jeshi la Polisi lilikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha usalama wa kutosha unakuwepo barabarani.
Ajali katika mchezo hazikukosekana lakini huduma ya kwanza ilikuwepo jamaa aliendelea na game na akawa mshindi wa tatu katika mbio ndefu. lakini licha ya kupata ajali alipewa baiskeli nyingine na hatimaye akawa mshindi wa tatu.
Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Ephaim Mafuru akizungumza kabla ya kutoa zawadi kwa washindi katika shindano hilo ambapo jambo kuu aliloahidi ni kwamba Kampuni ya SBL itaendeleza udhamini wake katika mashindano hayo na kuchukua changamoto mbalimbali zilizotolewa na walizoziona katika mbio hizo zilizoanza Busanda Shinyanga na kuhitimishwa katika eneo la kilima cha hospitali ya Bugando ambapo kwa wanaume mkimbia kutoka timu ya Arusha Richard Laizer akifuatiwa na Mindi Mwagi kutoka Shinyanga na mshindi wa tatu alikuwa Saidi Jumanne wa Arusha.
Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya simu Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza akimkabidhi zawadi y ash. Mil 1.5 mshindi wa kwanza wa mbio ndefu za baskeli za kilometa 196 mara baada ya kuibuka kinara katika mbio hizo zinazojulikana kama Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge, kushoto ni Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Ziwa Steven Kingu watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Masoko Kampuni ya Bia ya Serengeti Ephraim Mafuru na Meneja wa Kinywaji kisicho na kilevi cha Malta Guiness Mauris Njowoka.
Mwenyekiti wa Chama Cha Baiskeli katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga, Elisha Elias akizungumza kwa niaba ya wanachama wa Chama hicho mara baada ya mashindano ya mbio za baiskeli kum alizika siku ya Jumamosi Vodacom Mwanza Open Cycle 2011.Kadhalika wadhamini wenza katika shindano hilo ambapo ameomba wadhamini wawafikirie katika kutoa nyenzo muhimu ikiwa ni pamoja na baiskeli za kizaza yaani zenye gia.
0 Comments